Mshambuliaji wa zamani wa Manchester United Dwight Yorke anaamini kikosi cha sasa cha United chini ya Ole Gunnar kinauwezo wa kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza.
Mchezaji huyo wa zamani kutoka Trinidad & Tobago anaamini kikosi cha Man Utd kimesheeni wachezai wenye ubora unaoweza kuwafanya kushindana na timu zinazowania ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza huku akisisitiza kuwa Man Utd ina viungo wazuri zaidi ya liverpool.

“Nadhani tuna wachezaji wanaoweza kuchukua ubingwa wa ligi kuu ya Uingereza, je wanacheza kama mabingwa? hapana, tukirudi nyuma msimu mitatu au minne wakati Leicester wanachukua ubingwa, unaweza kuona wachezaji waliokuwa nao na wachezaji tulionao sisi, tunwachezaji wazuri wanaoweza kuchukua ubingwa.”
“Tuna kikosi kizuri, tuna walinzi imara, tuna golikipa bora na washambuliaji hatari, watu wanazungumza kuhusu viungo, huwezi kuwa na timu iliyokamilika, nikiangalia timu ya Liverpool pasipo kuwavunjia heshima katikati wana Henderson, Keita na mwingine simkumbuki ambaye walicheza nae wakati walipotufunga.”
“Huhitaji kuwa na kikosi kilichokamilika ili uweze kchukua ubingwa, ila unahitaji watu wanaoweza kubadilisha matokeo na kutawala mchezo, tuna Cristiano Ronaldo, Edinson Cavani, Paul Pogba na Raphael Varane ni uwendawzimu kuona nafasi tulipo, ni kweli inavunja moyo kuangalia na ni ngumu kukubali pia.” Alisema Yorke
Manchester United watarudi tena uwanjani baada ya mapumziko ya kimataifa na kusafiri kwenda kucheza na Watford tarehe 20 novemba.
Unawezaje kuikosa hii! njia rahisi ya kutengeneza mkwanja katika kasino maridhawa za meridianbet. Muda wa kufurahia na kutengeneza mkwanja ipo mikononi mwako unasubiri nini?


