Usajili: Ya Lovren na Liverpool

Lovren awatahadharisha Majogoo, mlinzi wa klabu ya Liverpool ameamua kufunguka na kuwapa uhalisia matajiri wake kwamba kurudi kwa mshindani mwenzake, Joe Gomez ndani ya kikosi hicho ni hatari sana kwa nafasi yake na kunaweza kumbadili akaporomoka. Mara nyingi wachezaji hupendelea ushindani wa namba lakini jambo hilo likimkosesha yeye kama mchezaji kwa nafasi kubwa huweza kumpotezea mwelekeo. Hadi sasa kuna fununu kutoka AC Milan kwamba klabu hiyo inaonesha matamanio ya kumsajili.

Nabil Fekir ataka kuhama, nyota na mchezaji wa Lyon ambaye amekuwa mchango mkubwa sana kwa kikosi hicho anaona kuna haja ya yeye kutimka klabuni hapo wakati huu. Alihusishwa sana na kujiunga na Liverpool msimu uliopita na kwa sasa nafasi hiyo kwake iko chini sana kutokana na nafasi ya kikosi hicho kwenye uhitaji wa wachezaji wa nafasi yake. Mbali na Liverpool, alikuwa akihusishwa kuwaniwa na United na hata Chelsea ambao hawana jeuri sokoni msimu huu.

Messi bado anamhitaji Neymar, nyota huyo wa klabu ya Barcelona anahitaji huduma ya mchezaji mwenzake huyo raia wa Brazil kwamba bado anathamini nafasi yake. Inasemekana kwamba amejaribu hata kumshawishi Rais wa klabu hiyo, Josep Maria Bartomeu kwamba angeachana na mipango ya kumsajili Antonie Griezman na kuangalia namna ya kumrudisha nyota huyo kikosini hapo. Hilo linatokana na mchango wa nyota huyo kwa kipindi alichokuwa akihudumu kikosini hapo.

Romelu Lukaku kuondoka, mshambuliaji wa klabu ya Manchester United ambaye hajaleta matunda ambayo kama klabu iliamini kuyapata kutoka kwake anaonekana mipango yake ya kutimka klabuni hapo ipo jikoni tayari. Amekuwa akihusishwa na klabu kubwa mbili ambazo zinaangalia nafasi ya kumnasa ili kufanya makubwa ndani ya klabu zao. Inter Milan wamevutiwa sana na nyota huyo lakini pia inasemekana Madrid nao wanaona nafasi yake japo kwa sasa wana wachezaji kama Jovic tayari kwenye nafasi yake.

Arsenal waonekana kukosa usajili, klabu ya Arsenal wanaonekana kukosa nafasi ya kumsajili kinda na nyota ambaye ameonesha uwezo mkubwa Sampdoria, Joachim Andersen. Lakini kwa sasa nyota huyo anawindwa na Tottenham ambao wameonesha mapendeleo ya aina yake kutaka kumsajili nyota huyo na mlinzi ambaye anaonekana atakuja kuwa bora sana katika soka. Arsenal wanaonekana kuwania saini ya Denis Praet na wana mapendeleo ya huko zaidi kwa kuridhishwa na utendaji kazi wa mchezaji huyo.

2 Komentara

    Hii ni habari mzuri sn Asante kw taarifa

    Jibu

    Hapatamfaa uko bora abaki tu

    Jibu

Acha ujumbe