Tanzania Yapanda Nafasi CAF, Yatinga Top 5 Afrika kwa Ubora wa Klabu

Tanzania imepanda kwa nafasi moja katika viwango vya ubora vya CAF na sasa kushika nafasi ya tano barani Afrika, hatua inayodhihirisha maendeleo ya soka la klabu nchini katika mashindano ya kimataifa. Awali Tanzania ilikuwa nafasi ya sita, lakini imeipita Tunisia ambayo sasa imeshuka hadi nafasi ya sita.

Tanzania Yapanda Nafasi CAF, Yatinga Top 5 Afrika kwa Ubora wa Klabu

Kupanda huko kumetokana na mafanikio ya klabu za Tanzania katika mashindano ya CAF Champions League na CAF Confederation Cup katika kipindi cha misimu mitano iliyopita, ambapo nchi imekusanya jumla ya pointi 82.5.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Mchango mkubwa wa pointi hizo umetokana na msimu uliopita ambapo Tanzania ilikusanya pointi 30, zikiwemo pointi 20 kutoka kwa Simba SC iliyofika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika, pamoja na pointi 10 kutoka kwa Yanga SC iliyofika hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika.

Tanzania Yapanda Nafasi CAF, Yatinga Top 5 Afrika kwa Ubora wa KlabuKatika misimu iliyotangulia, Tanzania iliendelea kufanya vizuri ambapo msimu wa 2023/2024 ilikusanya pointi 24 na msimu wa 2022/2023 ikipata pointi 21, hali inayoonyesha mwenendo mzuri wa klabu zake katika mashindano ya kimataifa.

Kwa mujibu wa viwango hivyo, Egypt inaongoza kwa pointi 190.5 ikifuatiwa na Morocco yenye pointi 142, huku South Africa ikiwa nafasi ya tatu na Algeria kushika nafasi ya nne.

Tanzania Yapanda Nafasi CAF, Yatinga Top 5 Afrika kwa Ubora wa KlabuMfumo wa upangaji wa viwango vya CAF huzingatia pointi zinazokusanywa na klabu kuanzia hatua ya makundi hadi fainali katika kipindi cha misimu mitano, ambapo mafanikio katika Ligi ya Mabingwa Afrika hupata uzito mkubwa zaidi kuliko Kombe la Shirikisho, jambo linaloifanya Tanzania kuendelea kunufaika na mafanikio ya hivi karibuni ya klabu zake.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.