Yanga: Tupo Tayari Kuwamaliza Al Hilal

UONGOZI wa Yanga umesema kuwa maandalizi ya mchezo wao wa kwanza dhidi ya Al Hilal utakaochezwa kesho kutwa Jumamosi uwanja wa Mkapa yamekamilika kwa asilimia 100 na kilichobaki ni Kwenda kushinda kwa idadi kubwa ya mabao.

Ofisa Habari wa Yanga, Ali Kamwe alisema kuwa wachezaji wote wapo tayari, benchi la ufundi chini ya kocha Mohamed Nabi, wameshamaliza kila kitu na wanasubiri dakika 90 za uwanjani ili ziwape matokeo wanayotarajia.

Kamwe alisema: “Tumeshazungumza sana juu ya namna ambavyo tunautaka mchezo huu kuliko michezo mingine yoyote ambayo ipo mbele yetu. Wachezaji wetu wapo tayari na wametuhakikishia mambo mazuri.
 
“Benchi la ufundi lipo tayari na limeshamilisha mipango yote na hadi kujua wapinzani wetu wanakuja na mbinu gani kwenye mchezo huo. Niwahakikishe Wananchi wenzangu kuwa hii mechi tunashinda.
 
“Niwaambie mashabiki muje kwa wingi kwenye uwanja wa Mkapa. Iwe, Iwe Mvua hawatatoka salama kwenye mchezo huu wakiwa hapa nyumbani na hata kwao.”

Yanga kesho kutwa watashuka kwa Mkapa na Al Hilal kucheza mchezo wao wa kwanza wa hatua ya kwanza wa ligi ya mabingwa. Kisha watasafiri hadi Sudan kucheza mchezo wa marudiano Oktoba 15.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.