Lois Boisson aweka rekodi Roland Garros kwa Kuingia Nusu Fainali

Lois Boisson ameendelea kuandika historia ya kipekee kwenye Mashindano ya French Open baada ya kumchapa mchezaji namba 6 kwa ubora duniani, Mirra Andreeva, na kufuzu hatua ya nusu fainali.

Lois Boisson aweka rekodi Roland Garros kwa Kuingia Nusu Fainali

Lois Boisson, anayeshika nafasi ya 361 kwa ubora duniani, alishinda kwa 7-6 na 6-3 mbele ya mashabiki wa nyumbani waliokuwa wakimshangilia kwa hamasa kubwa katika uwanja wa Roland Garros.

Akiwa haamini mara baada ya ushindi wake mkubwa, Boisson alianguka juu ya uwanja wa udongo kwa furaha kubwa sanahuku umati wa mashabiki ukilipuka kwa shangwe na kumshangilia.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa.

Lois Boisson aweka rekodi Roland Garros kwa Kuingia Nusu Fainali

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 22 sasa anakuwa mchezaji wa kike wa nafasi ya chini zaidi kuwahi kufika nusu fainali ya Grand Slam katika kipindi cha miaka 40, na ni wa tatu tu tangu 1980 kufika hatua hiyo katika mashindano yake ya kwanza makubwa (Grand Slam), baada ya Monica Seles na Jennifer Capriati.

Lois Boisson pia anakuwa mchezaji wa kwanza aliye nje ya 300 bora duniani kuwahi kuwashinda wachezaji wengi walio kwenye viwango vya 10 bora katika mashindano hayo tangu Serena Williams alivyofanya hivyo Chicago mwaka 1997.

Kwa ushindi huu, Lois Boisson anatarajiwa kupanda juu zaidi kwenye viwango vya ubora duniani, kwani baada ya kuingia nusu fainali amefanikiwa kupanda mpaka namba 68 ya ubora duniani.

Lois Boisson aweka rekodi Roland Garros kwa Kuingia Nusu Fainali

Kwenye mchezo huo wa kufuzu nusu fainali, Andreeva alianza vyema seti ya kwanza akiwa mbele kwa 3-1 na baadaye 5-3, lakini Boisson alijizatiti na kulazimisha sare (tie-break), na hatimaye kushinda mbele ya mashabiki wa nyumbani. Katika seti ya pili, licha ya Andreeva kuongoza 3-0, Boisson alirudi kwa kasi ya ajabu, akishinda gemu sita mfululizo na kufuzu kwa nusu fainali.

“Ni kitu cha ajabu. Asanteni kwa kunisapoti namna hii, sina maneno. Nilijikuta nikikimbia sana mwanzoni lakini nilipigana kweli katika seti ya kwanza. Nilipoanza seti ya pili nilihisi nimeishiwa nguvu, lakini nilijikaza na nikamaliza kazi.” Alisema Boisson.

Lois Boisson sasa atakutana na mchezaji namba 2 kwa ubora duniani, Coco Gauff, Kwenye hatua ya nusu fainali. Gauff alimshinda Madison Keys kwa seti tatu baada ya kupoteza ya kwanza, na kujihakikishia nafasi yake katika hatua ya mwisho ya mashindano hayo siku ya Jumatano.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.