MLS Yapanga Kutawala Soka Duniani Kupitia Fursa ya Kombe la Dunia

Ligi Kuu ya Marekani MLS, imeeleza mipango ya kutumia fursa ya Kombe la Dunia kuongeza umaarufu wake kimataifa, wakati United States ikiendelea na maandalizi ya kuwa mwenyeji mwenza wa michuano hiyo.

MLS Yapanga Kutawala Soka Duniani Kupitia Fursa ya Kombe la DuniaMaafisa wa soka wamesema ni muhimu kwa klabu za MLS kuvutia mashabiki kutoka nje ya nchi ili kunufaika na ukuaji mkubwa wa soka nchini humo.

Bila kusahau meridianbet ndio wakali wa ODDS KUBWA, Machaguo zaidi ya 1000 na kila kitu ukitakacho. Bashiri kijanja hapa  

Kwa mujibu wa rais wa CONCACAF, Victor Montagliani, lengo ni kuona mashabiki wa MLS wakienea duniani kote. “Nataka kuona mashabiki wa Atlanta United wakiwa London na Ujerumani,” alisema, akisisitiza umuhimu wa kupanua soko la ligi hiyo nje ya Marekani.

MLS Yapanga Kutawala Soka Duniani Kupitia Fursa ya Kombe la DuniaKamishna wa MLS, Don Garber, amesema mustakabali wa ligi hiyo uko katika kupanua wigo wa biashara na mashabiki nje ya Marekani na Canada. “Tunacheza mchezo wa kimataifa lakini kwa muda mrefu tumekuwa ligi ya ndani pekee. Sasa tunahitaji kupanua mipaka yetu,” alisema Garber.

Hata hivyo, changamoto kubwa ni ushindani kutoka kwa vilabu vikubwa vya Ulaya kama Real Madrid na Manchester United, ambavyo vina historia ndefu na mashabiki wa kizazi hadi kizazi. Tofauti na Ulaya, MLS ina kikomo cha mishahara, ingawa huruhusu wachezaji nyota maalum kama Lionel Messi kusajiliwa kwa masharti ya kipekee.

MLS Yapanga Kutawala Soka Duniani Kupitia Fursa ya Kombe la DuniaGarber pia aligusia uvumi wa uwezekano wa kumvutia Mohamed Salah, akisema: “Sidhani kama bado tunahitaji mikataba mikubwa ya aina hiyo. Zamani tulikuwa tunawashawishi wachezaji waje, lakini sasa hali imebadilika.” Hata hivyo, alikiri angependa kumuona nyota huyo akicheza MLS.

MLS Yapanga Kutawala Soka Duniani Kupitia Fursa ya Kombe la DuniaKatika hatua nyingine, MLS inapanga kubadili mfumo wa msimu ili uendane na kalenda ya kimataifa pamoja na kutumia FIFA World Cup kama jukwaa la kuvutia mashabiki wapya. Maafisa wanaamini kuwa miundombinu bora ya viwanja na vituo vya mazoezi itawavutia wachezaji na mashabiki kutoka mataifa mbalimbali kuendelea kufuatilia ligi hiyo baada ya mashindano kumalizika.

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.