KASHFA YA RUSHWA KOMBE LA DUNIA LA MWAKA 2022

Waendesha mashtaka wamefungua upya mashtaka ya kupewa rushwa waliyopewa Viongozi wa kamati kuu ya utendaji ya Fifa ili kuichagua Qatar kuwa wenyeji wa kombe la dunia kwa mwaka 2022. Juma tatu ya wiki hii mahakama  ya Brooklyn malalamiko yaliyofunguliwa na Nicolas Leoz yanasema kwa kipindi kile aliyekua Raisi wa shirikisho la mpira wa miguu la Marekani ya kusini na Raisi wa Zamani wa wa shirikisho la mpira la nchini Brazil bwana Ricardo Teixeira alipokea Rushwa ili kuwapigia kura Qatal kwenye kikao cha wakurugenzi wakuu wa Fifa wa Mwaka 2010.

Nicolas Leoz

Lawama hizo pia zimemkuita Jack Warner wa nchini Trinidat Na Tobago ambae nae alikua Raisi wa Body ya uongozi wa Marekani ya kaskazini na kati (CONCACAF) ambae alipewa zaidi ya dola milioni 5 kama Rushwa ili kuwapigia Urusi kuwa wenyeji wa kombe la dunia la mwaka 2018.

Raisi wa shirikisho la mpira la Guantemala Rafael  Salguero aliahidiwa dola milioni 1 ili nayeye apigie kura Urusi kuwa mwenyeji wa kombe la dunia. Na kwa mujibu wa mashataka hayo vitendo vya Rushwa vilivyo ripotiwa vimefikia 53.

Qatal ilishinda haki ya kusimamia na kuandaa Kombe la Dunia kwa mwaka 2022 kwa kura 8 kati ya 14 na ilipofika mwezi Disemba mwaka 2015 Kiongozi wa Taifa la Qatar alisema ni ubinafsi na upinzani ndio unafanya wao washukiwe kutoa Rushwa.

N mwezi Juni mwaka 2017 FIFA nao wakatoa tamko kwa report ya Michael Garcia na DR Cornel Brobely inayohusu udhabuni wa mwaka 2018/2022 wa Kuandaa kombe la Dunia na ripoti hiyo ikisema hakuna ushahidi wa aina yoye unayo onesha kua Qatar na Rusia walihusika na Tuhuma hizo

 

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.