Curtis Jones- Kizazi Kipya cha Viungo Wa Kati

Kipaji mujaarabu cha Jack Wilshere kiliwashitua wengi ,kiliwaacha midomo wazi kina Xavi Hernandez na Andres Iniesta pale Emirates katika mechi ya UEFA Champions League . Kuanzia wakina Scott Parker , Steven Gerrard , Frank Lampard , Paul Scholes na wengine wengi ni ngumu sana kumuona kiungo muingereza ambaye ni Stylish yaani anaecheza kwa sanaa , anaechora ramani inayovutia kama walivofanya kina Ricardo Kaka au Rivaldo pale Brazil . Siku zote waingereza wanacheza soka la mahesabu makubwa sababu wana mpira wa kufundishwa sanaa , Amerika Kusini kuna vipaji sanaa bila ya shule hakuna Academy nyingii kule kama Ulaya.

Jack Wishere

Kuna wachezaji wanacheza mpira wa sanaa yaani wanacheza mpira unaovutia na kuna wengine wanacheza mpira mahesabu , Andres Iniesta anacheza mpira wa sanaa anavutia kumtazama , Zinadine Zidane alikua anacheza sanaa licha ya matokeo anakupa burudani . Frank Lampard hana sanaa anakupa matokeo kwa njia yoyote ,Steven Gerrard hana mpira wa mvuto ana mpira wa kazi , Wayne Rooney alikua havutii kuanzia yeye mpaka stahili ya uchezaji ni nadra kwa Rooney kumpiga mtu kanzu , kumpiga tobo la aibu ila atapiga umbali wowote , atapiga faulo na kufunga yaani atafanya vitu vyote vyoote vya muhimu uwanjani.

Michael Owen hakua na sanaa alikua na kasi na clinical finisher ( mmaliziaji makini ) ,alianza Adam Lllana wakaja wakina Jack Greenlish na James Madson na wengineo waingereza wameanza kupata wasanii kwenye mpira yaani watu wanaokuvutia uwatazame , watu wa sanaa na mafundi wanakuja na wanaongezeka . Ukiachana na watu wote pale Liverpool utamkuta dogo wa kuitwa Curtis Jones nadhani mashabiki wa Liverpool wataelewa zaidi , kipaji halisi na murua kinachokuja kuushangaza uso wa dunia miaka kadhaa inayokuja Anfield itasimaa ikishuhudia kipaji madhubuti na mujaarabu kikiwaburudisha kops katika jukwaaa la Sir Kenny Daglish na mengine maarufu.

Tangu zama inajulikana Liverpool ni timu ya kiingereza yaani timu ya wagumu , inakusanya viungo wagumu wapiganaji wanaocheza mpira wa mahesabu makubwa . Xabi Alonso alitumia akili na mahesabu makubwa uchezaji wake ila hakua na sanaa , Steven Gerrard alikua mpiganaji sanaa na mwenye mahesabu lakini hakua na sanaa . Mshabiki wa Liverpool walipagawa na ujio wa Phillipe Coutinho sanaa sio kwamba hawajawahi pata kiungo bora waliokuwepo wengi tena zaidii yake lakini hawakua na stahili kama yake hawakua na sanaaa , akaja Adam Lallana na sasa wana Naby Keita kifupi wamenogewa . Sasa wanamleta Curtis Jones wameamua wamtengeze wao….

 

Curtis Jones

Curtis Jones ni mwanasanaaaa halisi anajua sanaa na anavutia pia , akiwa anacheza unaweza sema sio Mwingereza anakupa kila kitu burudani na matokeo mali makini inapatikana pale melwood . Jones ni moja ya vijana kipenzi wa Jurgen Klopp taratibu anaanza kupewa dimba , taratibu ameanza dakika kadhaa timu ya wakubwa analetwa taratibu duniani , Jurgen Klopp ameamua kumfungulia dunia kua anachotaka . Mashabiki wa karibu wa Liverpool Fc wanaelewa na wanamtambua sanaa huyu jamaa katika ligi za watoto pale Uingereza wanalitambua hili dinii , mashabiki wake wanampenda sanaa Naby Keita burudani makini kutoka Africa na watampenda zaidii Jones na wanaamini ndege akiingia ndani mwako haina haja ya manati.

5 Komentara

    Nikijana mdogo na anajua mpira aongeze juhudi ili awe tegemezi

    Jibu

    Ninamuamini sana kiungo muhimu

    Jibu

    Namkubalii sana huyoo kijana makini

    Jibu

    Kiungo hatari sana

    Jibu

    Mgoli na baba zetu Everton ulikuwa sio poa

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.