Mshambuliaji wa Ujerumani Timo Werner ameudhika kufuatia timu yake kuruhusu goli la dakika za majeruhi na kufanya mchezo kumalizika kwa 1-1 dhidi ya Spain katika michuano ya Nations League.
Werner alifunga goli la kuongoza dakika ya 51 ya mchezo Ujerumani wakiwa wanatafuta ushindi jijini Sturttgart siku ya Alahamisi, lakini Jose Gaya wa Hispania aliisawazishia timu yake dakika ya 95.
Nyota huyo wa Chelsea Timo Werner, ambaye anajiandaa kwaajili ya msimu wake wa kwanza akiwa Stamford Bridge baada ya kutua akitokea RB Leipzig, ameonesha kutolizishwa na matokeo kwani Ujerumani ilikuwa ikihitaji ushindi katika mchezo huo.
“Ni maudhi kwa sababu tumecheza kwa bidii kubwa sana,” Werner alisema baada ya mchezo kuisha.
“Baada ya goli tuliruhusu sisi wenyewe kurudi kucheza nyuma na kufanya wapinzani wapate nafasi kadhaa upande wetu.”

Kwa Matokeo hayo yanaacha Ujerumani iendelee kutafuta ushindi wao wa kwanza katika michuano hiyo baada ya kutoa sare mbili na kupoteza mchezo mmoja mwaka 2018-19.
Kocha mkuu wa Ujerumani Joachim Low aliongeza: “Nimeridhika na nilichokiona, vijana wetu wametuonesha walichokua nacho mpaka mwisho.
“Kwa upande wangu ni muhimu kutowaruhusu Spain kucheza na maoni yangu tulikuwa na nafasi nyingi, lakini kipindi cha pili hali ilikuwa ngumu kidogo.
Nyota wa Atalanta Robin Gosens pia alicheza mchezo wake wa kwanza akiwa na timu ya taifa ya Ujerumani na ndiyo aliyetengeneza asisti ya goli la Werner aliiambia UEFA.com “Ulikuwa ni usiku maalumu, mchezo wangu wa kwanza kucheza kama beki tatu, nafasi ninyocheza nikiwa Atalanta kwa hiyo ilikuwa rahisi kuimudu.
SHINDA NA HI LO
Sasa hii ni rahisi zaidi kupata USHINDI! Unatabiri karata ipi ipo chini au juu, kisha unakusanya mkwanja wako.


magdalena
spain wameniudhi sana jana wamejua kunichania mkeka wangu
Ester jackson
Hii inaonyesha kuwa wachezaji wa Chelsea msimu huu hawataki kabisa mchezo sio Werner tu hata sisi mashabiki kutokana na usajili tulio nao tunataka ushindi zaidi lakini kama Chelsea wakiongeza mabeki na kumleta kipa mwingine tutakuwa tumekamilika kila idara ila hasaivi bado ingawa tunawachezaji wazuri
[email protected]
Matokeo co mazr upande wao
Sadick
Kocha wa Joakim Low anatakiwa kujitazama,hana jipya,Ujerumani inashuka viwango badala ya kupanda#meridianbettz
Khadija
Chelsea wakiongeza mabeki na kumreta kipa mwengine tutakuwa tumekamilika kila idara ingawa sasahiv tunawachezaji wazur
felister
huo ndo mpira inabidi akubaliane na matokeo tu haina jinsi sio yeye peke yake aliyekerekwa lakini hatuna budi
Mwajumah
Wachezaji wa chelsea inaonyesha hawataki kabisa mchezo sio werner tu ata ss mashabiki#Meridianbettz
Fatina mfingi
Ndo matokeo hayo unabudi kukubariana nayo!
Mwanahamisi
Matokeo hayalizishi
Caroline
Huu sio muda wa kulaumiana yaliyotokea yametokea.waangalie walipokosea wajirekebishe
Sauda
Wakaze buti, matokeo hayaridhishi
Ernest
Kijana bado hajajifunza tuu kuwa mpira ni dakika 90?
Tatu
Timo Werner naona ajakubaliana na matokeo ya timu yake ya kutoka sale hii inaonyesha jinsi gani anamapenzi ya dhati na timu yake
Adelta
Mashabiki hatujafurahi matokeo
@meridianbettz
Dorophina
Hayo ndio matokeo inabidi wakubaliane na hali asiye kubali kushindwa sio mshindani
Lydia Emmanuel Magoti
Hayo ndio matokeo lazima wakubaliena nahali halisi kila mtu kapambana kwajudi zao zote nampila kila mtu kaupika kwaio kila mtu lango lake lilikaza kwahio kilamtu akubali Kama alishindwa kuliona lango lamwenzie kupataushindi wamoja kwamoja
rama
ndo moja wapo ya matokeo ya mpira
Shafii
Inapaswa aelewe kwamba mpila unamatokeo matatu ushindi,kupoteza na sare kwaiyo wajipange kwa mechi ijayo.
[email protected]
Ndio matokeo inabudi kukubaliana nayo
Nasra
Hakuna namna hapo ni kkubali matokeo tu
Genia Sikaluzwe
Ni lazma wa kubaliane na matoke
Furahav
Ndo mpira ulivyo.
Issa
Germany ya kipind hiki ni moto sana
Rose kapinga
Juhudi za ziada zinaitajika na mazoezi ya kutosha kama wanataka kubadili matokeo!!!
Hope mwaikuka
Mpira huko na matokeo matatu kubali tu
Saupha mohamed
Mpira kazima uwe na matokeo ya kushinda au kushindwa so akubali matokeo
Shani
Werner game ya jana uzoef wa Spain uliwafany wapate goli dakika ya mwisho
farida ahmadi
Mpira dakika 90 hiyo ni kawaida kikubwa kujiweka sawa katika kikosi
Neema
Ndio mchezo ulivyo akubaliane na matokeoo
Sabrina
Mpira unamatokeo matatu kufunga,kufungwa na kusuruhu na asiekubali kushindwa sio mshindani
Povel
Mpr dk 90 na una matokeo matatu kufungwa kushinda sare co kama utakubaliana na matokeo yyte utakuwah co mshindani
Amiri Kayera
Ndo matokea ya mpila kila Mt anatak ushind
Isaya massawe
Bahati haikua yakwao japo walicheza vizuri sana
Gabriel
Chelsea msimu huu hawataki kabisa mchezo sio Werner tu hata sisi mashabiki kutokana na usajili tulio nao tunataka ushindi zaidi lakini kama Chelsea wakiongeza mabeki na kumleta kipa mwingine tutakuwa tumekamilika kila idara ila hasaivi bado ingawa tunawachezaji wazuri
warda
Mambo ya sare Mie siyapendagi
Frank
Ni matokeo ilimpasa akubaliane nayo