NBA: Lakers Kucheza Fainali dhidi ya Heats

Kunako msimu wa NBA, michezo ya Eastern na Western Conference imemalizika na sasa washindi – LA Lakers na Miami Heats kuanza kuchuana ili kumpata mbabe wa NBA 2020.

Katika mchezo wa Eastern Conference, Miami Heats walikuwa wakichuana na Boston Celtics. Mchezo ambao ulikuwa na jumla ya michezo 7 na umehitimishwa kwa michezo 6 baada ya Miami Heats kuibuka kidedea kwa matokeo ya 4-2 katika michezo hiyo.

Miami Heats ambao ni washindi wa NBA mara 3, sasa wanatinga hatua ya fainali kwa mara ya kwanza tangu mwaka 2014. Mchezo wao uliomalizika kwa ushindi wa pointi 125-113 umepeleka kilio kwa Boston Celtics ambao wanapoteza fainali ya 3 mfululizo.

Wachezaji wa Miami Heats wakikabidhiwa kombe la Eastern Conference

Bam Adebayo alikuwa shujaa wa Heats kwa kupachika pointi 32 na kucheza mipira 14 iliyokufa. Adebayo amejisafisha kibabe kwa kile alichokifanya katika mchezo wa 5 ambapo aliwagharimu wachezaji wenzake.

“nilipaswa kujipanga kivingine na kuonesha kile ninachohitaji kuwa na nimefanya hivyo usiku wa leo. Kuwepo katika hali ile na kujifunza kutoka pale, kuisaidia timu kushinda fainali na kusonga mbele, ni kitu kikubwa kwangu.” amesema Adebayo.

Kwa upande wa LA Lakers, LeBron James ameisaidia timu yake kufika fainali ya NBA baada ya miaka 10 kwa ushindi wa pointi 117-107 dhidi ya Denver Nuggets. 

Ushindi wa jana, umewapatia matokeo ya jumla ya 4-1 katika michezo 5 na sasa wametinga hatua ya Fainali ya NBA 2020.

LeBron James alikuwa shujaa wa Lakers kwa kupachika pointi 38 na kucheza mipira 16 iliyokufa huku akitoa pasi 10 za magoli.

Wachezaji wa LA Lakers wakifurahia kombe la Western Conference

LaBron James anakuwa ni mchezaji wa 4 wa kucheza fainali 10 za NBA na hii ni mara yake ya kwanza akiwa na Lakers.

“Ninafuraha kubwa kuwa sehemu ya timu hii na kuisaidia kurudi katika nafasi yake,ambayo ni kucheza kwenye fainali.” amesema LeBron James.

Mchezo wa kwanza wa fainali utachezwa Jumatano.


Beti kwa Kitochi Kushinda 300,000,000!

Unajua kuwa unaweza kushinda milioni mia tatu kwa buku tu? Ndiyo! Unaweza kushinda kwa kupiga *149*10# na kubashiri. Ingia mchezoni!

Soma Zaidi

38 Komentara

    NBA mambo ni moto. VITA ya james le Bron vs Bam Adebayo🔥🔥🔥🔥🔥🔥

    Jibu

    lakers wapo vizuri sana wakiitumia vizuri nafasi yao wanaweza kuibuka na ubingwa

    Jibu

    Wapo vizuri

    Jibu

    Namuona LeBron kama MVP ndani ya NBA

    Jibu

    NBA kumenoga

    Jibu

    Laker wapo vizuri ili pambano litakuwa la nguvu

    Jibu

    Mchezo utakua mgumu sana kwa Lakers maana heats wapo vizuri sana wanamolali ya kuchukua ubingwa toka 2014 hii nafasi himekua kama bahati kwao sijui kama wataipoteza

    Jibu

    NBA sio mchezo lakers hawamwachi mtu salama

    Jibu

    NBA kumepamba moto patakuwa apatoshi

    Jibu

    NBA kumekucha

    Jibu

    Lakers naona kama ndio watakao pata ubingwa

    Jibu

    Wapo vizuri

    Jibu

    NBA Mambo mazuri

    Jibu

    Wapo vizur

    Jibu

    NBA kumenoga

    Jibu

    Naiaminia sana Lakers maana kiwango chai kipo juuu

    Jibu

    Mambo yanazidii kunoga

    Jibu

    Asnt kwa taarif

    Jibu

    LeBron na Davis wanaweza kuuzuia moto wa hearts

    Jibu

    Wapo vizuri

    Jibu

    Wacha ww

    Jibu

    NBA Mambo mazuri

    Jibu

    Gud news

    Jibu

    mambo ni moto na meridianbet

    Jibu

    NBA imepamba moto kwakweli

    Jibu

    Utakua mpambano mkali

    Jibu

    Safiii

    Jibu

    Kila la kheri kwao

    Jibu

    Lakers ni noma sana

    Jibu

    Lakes jeshii

    Jibu

    Lakes nomaa

    Jibu

    Kila lakheri kwao

    Jibu

    Kumenoga NBA

    Jibu

    Hatariiii

    Jibu

    wapo vizuri

    Jibu

    NBA kumekucha

    Jibu

    NBA mambo ni moto. VITA ya james le Bron vs Bam Adebayo

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.