Rais wa Napoli Aurelio De Laurentiis amesema kwamba jina la uwanja wa klabu linatakiwa libadilishwe kwa heshima ya kumenzi mkongwe Diego Maradona baada ya kufariki siku ya Jumatano.

Maradona ni mchezaji bora wa dunia wa muda wote, amefariki akiwa na umri wa miaka 60 baada ya kugundulika kuwa na shambulio la moyo, chama cha mpira nchini Argentina (AFA) kilithibitisha katikati ya wiki.
Mshindi huyo wa kombe la dunia akiwa na Argentina alifurahia mafanikio mbalimbali akiwa Naples,ambako aliiongoza Napoli kutwaa taji la Serie A mwaka 1986-87 na 1989-90.
Kama mashabiki wa Napoli na wananchi wa Naples wameshitushwa na kifo cha mkongwe Maradona na Rais wa De Laurentiis amesema dimba la Stadio San Paolo linatakiwa libadilishwe jina na kuitwa jina la gwiji huyo kama ishara ya kuheshimu mchango wake.
“Itakua wazo zuri kulibadili jina la uwanja na kuuita San Paolo-Maradona ni jambo ambalo tunaweza tukalifikiria,” De Laurentiis aliiambia RMC Sport.
Meya wa jiji Luigi de Magistris pia alitweet: “Acha tuite dimba la San Paolo, Diego Armando Maradona!!!”
Gennaro Gatuso na timu yake ya Napoli wataiongoza Rijeka katika dimba la San Paolo siku ya Alhamisi kwenye michuano ya Europa League katika kundi F.
Napoli wapo nafasi ya pili katika jedwali la Europa League wakiwa nyuma ya AZ Alkmaar kwa tofauti ya magoli.
“Ningependa kuona sura ya Maradona ndani ya uwanja wakati wote wa mchezo siku ya Alhamisi,” alisema De Laurentiis.
Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.



Povel
Kila la kheri. Jina hlo la kumuenzi nguli mkongwe wa soka wa dunia
Ester jackson
Itakuwa kumbukumbu zuri sana nafikiri jina lake haliwezi kupotea kutokana na heshima hiyo kama atapewa
Sadick
Utakuwa uamuzi sahihi kwa Napoli na Mashabiki kwa ujumla maana bila Diego Maradona Napoli isingechukua ubingwa wa ligi ya Italy na ndiko alikoanza tatizo la kutumia madawa ya kulevya
Sauda
Imetulia hiyo!!!
Adelta
Kila la kheri mkongwe wa soka
magdalena
kumbukumbu isiyofutia hii
Fatina mfingi
Safi
Tatu
Kumbu kumbu nzuri
Shakila mrope
Kila ka kheri
Lydia Emmanuel Magoti
Nivizuri Sana kuchukuwa uwamuzi wakuita jina hilo
Dorophina
Wamefanya Jambo jema sana kuweka kumbu kumbu ya legendary huyo maradona
Samira
Msiba mkubwa sana kwenye soka R.I.P Maradona
Khadija
Safi
Saupha mohamed
Jambo zuri sana
aisha
Imeisha iyooo
Genia Sikaluzwe
Jambo jema sana
Hopemwaikuka
Such a wonderful news
samiah
Nivizuri
Tahiya
Ni habari njema
warda
Wanastahili kufanya hivyo kwa kweli