Ulimwengu wa soka umepoteza Legendari, na kumbu kumbu yake haitafutuka. Diego Maradona ataendelea kutawala. Huu ni mtazamo wa raisi wa Inter ambao unaungwa mkono na wapenzi wengi wa soka.

Makamu wa rais wa Inter Javier Zanetti amesisitiza kuwa uwepo wa Diego Maradona ‘utahisiwa kila wakati katika kila uwanja wa mpira na katika viwanja vyote vya soka nchini Argentina.’

Diego Maradona

Mechi ya Inter dhidi ya Real Madrid kwenye Ligi ya Mabingwa haikukaa kabisa kichwani mwa Zanetti bila shaka mawazo yote yalikuwa kwa Maradona, legendari aliyeaga dunia akiwa na umri wa miaka 60.

“Maradona alimwakilisha kila mtu anayependa mpira wa miguu. Alikuwa wa kipekee, jinsi alivyotufurahisha uwanjani, “Zanetti alizungumza na Skysport

“Diego alikuwa amezoea pia kushughulikia changamoto hizi zote na kusimamia misimamo yake. Hatuwezi kuamini kwamba ni kweli, Diego ameenda. Ni wakati wa kusikitisha kwa kila mtu anayependa mchezo huu.”

Zanetti alikuwa kijana wakati Argentina ikishinda Kombe la Dunia na Maradona mnamo mwaka 1986.

“Nilikuwa na umri wa miaka 13, ilikuwa moja ya wakati mzuri sana maishani mwangu. Kuona Argentina ikishinda Kombe la Dunia na kuona kile Diego Maradona alikuwa akifanya katika mashindano hayo ilitupa furaha kama kubwa kama hiyo.”

“Diego alizidisha mapenzi yake makubwa kwa mchezo huu na uwepo wake utahisiwa kila wakati katika kila uwanja wa mpira, kila kila kijiji na kona ya barabara ambayo mpira unachezwa nchini Argentina.”

Diego Maradona

Anguko la Diego limetawala vichwa vya habari za michezo kila kona, huyu alikuwa mwamba wa soka. Mchango wake hautakuja kusahaulika na historia yake itaendelea kuandikwa daima. Andre Villas-Boas amesema FIFA pia wanapaswa kuiondoa namba 10 kwenye namba za timu kwa ajili ya kuilinda heshima ya nyota huyu. Buriani Diego Maradona


 

USICHELEWE KUKAMATA MKWANJA HUU!

Hadi 130,000,000 TSH Kutolewa kwa washiriki wa shindano la Playson Cashfall. Unaipata kwenye Kasino ya Mtandaoni ya Meridianbet Pekee. Jisajili sasa, kisha ingia mchezoni kabla ya Novemba 29.

Meridianbet Tanzania Casino

SOMA ZAIDI

20 MAONI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa