Kevin Durant Kuendelea Kukaa Nje ya Uwanja.

Mchezaji nyota wa timu ya Brooklyn Nets – Kevin Durant [KD] ameripotiwa kuendelea kukaa nje ya uwanja kutokana na majeruhi.

KD hajarejea uwanjani tangu alipocheza dhidi ya Golden State Warriors (Februari 13 2021), hii ni baada ya kuumia nyonga ya kushoto.

Mchezo wa Nets vs Boston Celtics leo usiku utakuwa ni mchezo wa 10 mfululizo kwa Kevin Durant kukosekana uwanjani.

Kocha wa Nets – Steve Nash amethibitisha KD atafanyiwa uchunguzi mwingine siku chache zijazo na mpaka sasa, haijajulikana ni lini mchezaji huyo atarejea tena uwanjani.

Durant (kushoto) akichuana na Stephen Curry (kulia) kwenye mchezo wa Nets vs Warriors (Februari 13, 2021)

[KD] hajacheza kwa mwezi mmoja. Haijalishi matokeo ya uchunguzi yatasemaje, bado tunahitaji muda ili kuhakikisha anaumaliza msimu huu akiwa imara zaidi.

“Kwa sasa anaendelea vizuri na tunaimani chanya na muelekeo alionao lakini tunapaswa kuchukua tahadhari kwa sababu ni mchezaji wa muhimu sana kwetu.” alisema Nash.

Durant hakusafiri kwenda Atalanta kwenye michezo ya NBA All Stars na badala yake alibaki Brooklyn chini ya uangalizi wa madaktari wake.


Ni Burudani Iliyokithiri na Mkwanja Nje Nje Katika Mchezo Halisi wa Chicago Gold.

Fanikisha malengo yako bila kuumiza kichwa, tengeneza mkwanja bila wasiwasi na kasino ya Meridianbet. Jiunge sasa Ufurahie Chicago Gold kasino.

CHEZA HAPA

9 Komentara

    Pole sana Kelvin utapona tu

    Jibu

    Duu pole yake

    Jibu

    Sorry for you

    Jibu

    Pole Key

    Jibu

    pole yake

    Jibu

    Pole yake kijana

    Jibu

    Pole yake

    Jibu

    Pole yake

    Jibu

    Durant pole

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.