Mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham atafanyiwa vipimo vya afya huko Roma siku ya Jumapili kuelekea kukamilisha uhamisho wa €40m (£34m/$47m) na klabu hiyo ya Italia.

Abraham atasafiri kwaajili ya kukamilsha uhamisho wa kudumu baada ya kuonekena kutokuwa kwenye mipango ya Thomas Tuchel.
Urejeo wa Lukaku huko Chelsea ungeweza kupelekea mchezaji huyo wa miaka 23 kutopata muda mwingi wa kucheza na klabu mwishowe imeamua kumuuza mchezaji huyo ambaye alikuwa amebakisha miaka miwili kwenye mkataba wake.
Abraham ameripotiwa kuwa atasaini mkataba utakao muweka Roma mpaka mwaka 2026 na anatarajia kupata mshahara wa €5m kwa mwaka.

Katika mkataba huo kunakipengele cha kumnunua tena kwa dau la €80m (£68m/$94m) baada ya kumaliza misimu miwili huko Stadio Olimpico ambako atakuwa chini ya kocha wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho.
Tammy alifanikiwa kuichezea Chelsea michezo 82 na kufunga mabao 30na kuisadia The Blues kushinda Ubingwa wa Ulaya kwa mara ya pili msimu uliyopita.
Unaanzaje siku yako bila kuwa na pesa, Meridianbet kupitia kasino zake za mtandaoni inakupa sababu ya kufanya siku yako kuwa njema. Mchezo maarufu wa Tiki Reward unaweza kukufanya milionea. Cheza sasa kibingwa!


