Tammy Kusafiri Mpaka Roma Kwaajili ya Vipimo

Mshambuliaji wa Chelsea Tammy Abraham atafanyiwa vipimo vya afya huko Roma siku ya Jumapili kuelekea kukamilisha uhamisho wa €40m (£34m/$47m) na klabu hiyo ya Italia.

Tammy Kusafiri Mpaka Roma Kwaajili ya Vipimo

Abraham atasafiri kwaajili ya kukamilsha uhamisho wa kudumu baada ya kuonekena kutokuwa kwenye mipango ya Thomas Tuchel.

Urejeo wa Lukaku huko Chelsea ungeweza kupelekea mchezaji huyo wa miaka 23 kutopata muda mwingi wa kucheza na klabu mwishowe imeamua kumuuza mchezaji  huyo ambaye alikuwa amebakisha miaka miwili kwenye mkataba wake.

Abraham ameripotiwa kuwa atasaini mkataba utakao muweka Roma mpaka mwaka 2026 na anatarajia kupata mshahara wa €5m kwa mwaka.

Tammy Kusafiri Mpaka Roma Kwaajili ya Vipimo

Katika mkataba huo kunakipengele cha kumnunua tena kwa dau la €80m (£68m/$94m) baada ya kumaliza misimu miwili huko Stadio Olimpico ambako atakuwa chini ya kocha wa zamani wa Chelsea Jose Mourinho.

Tammy alifanikiwa kuichezea Chelsea michezo 82 na kufunga mabao 30na kuisadia The Blues kushinda Ubingwa wa Ulaya kwa mara ya pili msimu uliyopita.


 

SHINDA NA TIKI REWARD KASINO

Unaanzaje siku yako bila kuwa na pesa, Meridianbet kupitia kasino zake za mtandaoni inakupa sababu ya kufanya siku yako kuwa njema. Mchezo maarufu wa Tiki Reward unaweza kukufanya milionea. Cheza sasa kibingwa!

Tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.