Bondia wa Ufilipino Manny Pacquiao amesema kwamba kazi yake ya ubondia imefika tamati ingawa wakuu wa timu yake ya Promosheni wamesema mazungumzo ya kustaafu kwake bado.

Bondia huyo wa miaka 42 alipoteza kwa Yordenis Ugas mwezi ulitopita na wengi wakitabiri kwamba huo ndiyo mwisho wake na huenda hilo ndiyo pambano lake la mwisho.
Pacquiao alikuwa Jumapili ametangaza nia yake ya kuwania urais wa Ufilipino mwaka ujao.
Bingwa huyo wa zamani wa uzito wa nane aliiambia Toni Talks kuwa amemaliza na ndondi.
“Kazi yangu ya ndondi tayari imekwisha,” Pacquiao alisema.
“Imefanywa kwa sababu nimekuwa kwenye ndondi kwa muda mrefu na familia yangu inasema kuwa inatosha.”
Lakini, mkuu wa Promosheni wa Pacquiao Sean Gibbons alisema mazungumzo yoyote ya kustaafu bado.
“Seneta ni mgombea wa urais na bado hajafanya uamuzi wowote juu ya maisha yake ya ndondi,” Gibbons aliiambia Yahoo Sports.
“Katika wiki chache zijazo atafanya uamuzi wa mwisho ikiwa atakuwa na zaidi au astaafu.”
Ni wakati wa ushindi mkubwa ukiwa na kasino bomba ya Lock a Luck, meridianbet wanakupa sababu ya ushindi, funga bahati yako ya ushindi ukiwa na mabingwa.


