Nyota wa Manchesster United Paul Pogba amepata majeraha akiwa kwenye mazoezi ya timu ya taifa ya Ufaransa wakijiandaa na kichezo ya kimataifa ya kufuzu kombe la dunia 2022 nchini Qatar.
Pogba alionekana akitoka mazoezi huku akiwa anachechemea huku akishika zaidi paja, kuna uwezokano asiwepo kwenye mchezo dhidi ya Kazakhstan na Finland baada ya kuonekana akitoka mazoezini siku ya jumatatu.

Video iliyoachiwa na kituoa cha MC Sport, Pogba alisikika kwa sauti kubwa akipiga kelele kuonesha kuwa ameumia baada ya kupiga mpira na mguu wake wa kulia na kutoka nj’e kwenda kwenye gari na kuondoka mazoezini.
Bado haijathibitishwa ni kwa ukubwa gani wa majeraha aliyopata, lakini inaonekana ni jeraha kubwa mpaka kumfanya asiweze kuendelea na mazoezi na kuondoka.

Man Utd inawafaransa wawili ambao waliumia wakiwa kwenye majukumu ya kimataifa ambao ni Anthony Martial na Raphael Varane ambao waliumia kwenye mapumziko ya oktoba, Varane alikosa michezo mitatu kabla ya kupata tena majeraha yaliyomuweka tena nj’e kwa mwezi mmoja tena, wakati Martial hajacheza mchezo wowote mpaka sasa.
Unawezaje kuikosa hii! njia rahisi ya kutengeneza mkwanja katika kasino maridhawa za meridianbet. Muda wa kufurahia na kutengeneza mkwanja ipo mikononi mwako unasubiri nini?


