NBA: Nuggets Wanapindua Meza

Mchezo wa 3 katika muendelezo wa fainali ya NBA Wesstern Conference umechezwa usiku wa kuamkia leo. Denver Nuggets walivaana na LA Lakers.

Kabla ya mchezo wa jana, Lakers walikuwa wanaongoza kwa matokeo ya 2-0. Msimu huu, Nuggets wameshaweka historia ya kupindua matokeo katika mechi 2 mfululizo. Walifanya hivyo dhidi ya Utah na LA Clippers.

Mchezo wa jana, Denver walishinda kwa pointi 114-106. Ushindi uliochagizwa na Jamal Murray aliyefunga pointi 28 pamoja na Jerami Grant pointi 26. Ushindi huu umetia doa safari ya ushindi wa Lakers katika michezo 6 mfululizo licha ya LeBron James kufunga pointi 30 na kutoa pasi 10 za magoli.

“Tupo kwenye haya mashindano. Tumewaonesha kwamba hatuendi popote. Ndicho wanachokifanya vijana wangu msimu huu wote.

“Ndio sababu kila mtu anatuzingatia, tunaendelea kuonesha uvumilivu wetu na kuendelea kucheza kwa umoja.” amesema kocha wa Nuggets – Michael Malone

Mchezo wa 4 utachezwa Alhamisi ya wiki hii. Kunako NBA Eastern Conference, Miami Heat anaendeleza ubabe dhidi ya Boston Celtics na sasa matokeo ni 2-1. Mchezo wa 4 kati yao utachezwa leo Jumatano.

Mshindi wa NBA Western Conference, atachuana na mshindi wa Eastern Conference ili kumpata bingwa wa NBA msimu huu.


FURAHIA KASINO YA MTANDAONI

Tembelea ardhi ya maajabu ushangazwe na mengi ikiwa ni pamoja na urahisi wa kujipatia utajiri kupitia Kasino ya Meridianbet.

Cheza Sasa

22 Komentara

    NBA kumenoga Mambo yanazid kupamba moto

    Jibu

    Naona wameanza vizuri kama kazi ipo acha tuone

    Jibu

    Wako vinzur

    Jibu

    Hongera kwao nuggets

    Jibu

    N.B.A nayo sasa Ivi Ina wafuasi wengi

    Jibu

    Wametishaa kinoma

    Jibu

    Mambo yanazidi kutaradady NBA

    Jibu

    wakipambana vizuri ipasavyo watapinfua kweli meza

    Jibu

    Ngoja tusubiri tuone matokeo

    Jibu

    Wako vizuri

    Jibu

    Wako poa

    Jibu

    Nuggenets walianza vizur mwisho lakers uzoefu uliwasaidia

    Jibu

    Wababe wanachuana!!

    Jibu

    Inakuwaje hadi wanapindua meza

    Jibu

    Watawezaa

    Jibu

    Nuggets ndio zao

    Jibu

    ngoja tuone matokeo

    Jibu

    Nuggets wanatukumbusha kutokata tamaa#meridianbettz

    Jibu

    Wapo vizuri

    Jibu

    Wanangu Lakers hawatoniangusha sina wasiwasi kabisa

    Jibu

    Mambo yanazidi kunoga

    Jibu

    Matokeo ndo yataamua

    Jibu

Acha ujumbe