Mambo si mambo kunako timu ya Golden State Warriors, kwa misimu miwili mfululizo, wanashindwa kufuzu hatua ya Play-Offs kunako NBA.
Warriors ambao wameendelea kuwa na msimu mbaya msimu huu, walijikuta wakiangukia pua kwenye michezo ya Regular Season na hivyo kucheza shindano fupi la Play-in tournament kama sehemu ya kuisaka tiketi ya kucheza Play-Offs.
Mchezo wa kwanza, Warriors walifungwa na LA Lakers baada ya LeBron James kupachika mpira wa three pointer zikiwa zimesalia sekunde 58 mchezo ule kumalizika. Kupoteza dhidi ya Lakers kuliwapa nafasi Warriors kuchuana na Memphis Grizzlies katika kuwania nafasi ya 8 kwenye msimamo wa NBA – Western Conference.
Hakika siku ya kufa nyani, miti yote huteleza. Warriors wameangukia pua mara nyingine baada ya kufungwa kwa pointi 117-112 katika mchezo uliochezwa kwa muda wa nyongeza.

Baada ya vuta n’kuvute nyingi, kama ilivyokuwa kwa LeBron James, Ja Morant alizamisha jahazi la Warriors kwa kupachika mpira wa alama 2 zikiwa zimesalia sekunde 4 mchezo kumalizika.
Licha ya Stephen Curry kupachika pointi 39 kati ya 112 za Warriors, Ja Morant alikuwa shujaa wa Grizzlies ambaye anaipeleka timu hiyo kwenye hatua ya mtoano kwa mara ya kwanza kwenye misimu minne.
“Ninapenda kucheza kunapokuwa na msukumo mkubwa, ninajiamini kwa kiasi kikubwa kwenye uchezaji wangu” alisema Morant.
“Inafedhehesha kwamba huu ndio mwisho na hivi ndivyo tunavyotoka” alisema Curry.
Michezo ya Play-Offs kunako NBA itaanza leo usiku ambapo Milwaukee Bucks watachuana na Miami Heat kwa upande wa Eastern Conference, LA Clippers watachuana na Dallas Mavericks kule kwenye Western Conference.
Zungusha na ushinde mkwanja wako papo hapo baada ya mzunguko kukamilika. Ni kugusa tu 🤑.
Shakila
Eeh pole yao
Magdalena
Wanatuangusha sana