Mpiganaji masumbwi uzito wa juu Deontay Wilder amesema anataka kupigana na Anthony Joshua bondia raia wa Uingereza mwenye asili ya Nigeria barani Afrika akiamini bado ni pambano namba moja.
Deontay Wilder ambaye hajapigana toka mwaka jana alipopoteza pambano dhidi ya mwingereza Tyson Furry, Lakini bondia huyo hivi karibuni ataingia ulingoni kupambana na na bondia Robert Helenius huku Brooklyn Marekani.Kurejea ulingoni kwa bondia huyo inakua ni safari yake ya matumaini ya kurudisha mikanda yote mikubwa inayoshikiliwa na mabondia Tyson Furry pamoja na Olexnder Usyk, Lakini wakati huohuo anataka mpambano na Anthony Joshua.
Pambano kati ya Deontay Wilder na Joshua lingekua pambano la namba moja duniani kama wangekutana hapo nyuma kabla ya mikanda yao kubebwa na Furry pamoja na Usyk.Pamoja na hivo bado Wilder anaamini hilo ni pambano namba moja duniani huku akipanga kulileta pambano hilo barani Afrika. “Ningependa kulileta pambano hilo Afrika. Bado ni pambano namba moja duniani kwa kila mtu. Kila niendako watu wananizungumzia mimi na Joshua” Alisema hayo wilder