Claotus Chama mchezaji wa klabu ya Simba amefanikiwa kua mchezaji bora wa mwezi wa nane wa mashabiki mdani ya klabu ya Simba inayotolewa na kampuni ya Emirate Alluminium.

Mchezaji huyo ambae amefanikiwa kunyakua tuzo hiyo baada ya kufanikiwa kucheza kwa kiwango bora ndani ya mwezi uliopita na kumfanya akawa bora na kunyakua tuzo hiyo.

chamaChama anakua mchezaji wa kwanza wa klabu hiyo kunyakua tuzo hiyo kwa msimu wa 2022/23 na tuzo hutolewa kila mwezi kwa mchezaji aliefanya vizuri ndani ya timu hiyo na hii sio mara ya kwanza kwa mchezaji huyo kua mchezaji bora wa mwezi wa klabu hiyo kutokana na ubora ambao hua anauonesha ndani ya timu hiyo.

Utaratibu wa kuchagua mchezaji bora hua unakua kwa mashabiki wa timu hiyo ambao wanapewa nafasi ya kupiga kura kupitia tovuti mbalimbali za klabu hiyo na kuweza kuchagua yupi mchezaji wao bora wa mwezi kama ambavyo wamefanya kwa mwamba wa Lusaka na kuchukua mchezaji huyo.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa