Karim Benzema na Dani Carvajal wote wapo kwenye shaka la kukosa mchezo ujao wa Real Madrid wa LaLiga dhidi ya Cadiz siku ya Jumapili katika dimba Estadio Santiago Bernabeu sababu ya majeraha.

Los Blancos watamenyana na kikosi cha Alvaro Cervera bila uwepo wa Luka Modric, Marcelo, Marco Asensio, Rodrygo, Gareth Bale na Andriy Lunin, ambao wote wamepatikana na COVID-19.
Carvajal amekuwa akipata muda wa kucheza chini ya Carlo Ancelotti,kwa upande wa Benzema alicheza dakika 45 kwenye mchezo wa derby dhidi ya Atletico Madrid na kufunga bao moja kabla ya kutoa nafasi kwa Luka Jovic.
Hii ina maana kwamba Ancelotti anaweza kukosa wachezaji kama wanane kwenye mchezo dhidi ya Cadiz, huku watatu kati yao wakiwa wakiwa na uhakika wa kucheza katika kikosi cha kwanza.
Real Madrid kwa sasa wanaongoza jedwali la LaLiga Santander, wakiwa na pointi 13 mbele ya Atletico Madrid na pointi 18 mbele ya Barcelona.
Fanya wiki yako iwe ya ushindi mkubwa ndani ya kasino za mtandaoni za meridianbet. Mchezo wa BURST THE BANK🔥🤑 ni moja kati ya mchezo pendwa unaowapa wachezaji mamilioni kila siku. Kwa dau dogo unashinda zaidi.


