Christensen: Tunahitaji Marekebisho Haraka Sana

Beki wa Chelsea Andreas Christensen amekiri kwamba klabu hiyo inahitaji kufanya marekebisho katika safu ya ulinzi haraka iwezekanavyo kabla mambo hajawa magumu zaidi.

Christensen: Tunahitaji Marekebisho Haraka Sana

Chelsea imeruhusu mabao saba kwenye michezo miwili iliyopita ilifungwa 4-1 dhidi ya Brentford katika Premier League wakati pia ilikubali kipigo cha 3-1 dhidi ya Real Madrid katika Ligi ya Mabingwa ikiwa ni hatua ya robo fainali.

Licha ya hali wanayopitia klabuni hapo Chelsea walikuwa wanafanya vizuri kabla ya mapumziko ya kimtaifa mpaka walikutana na Brentford.

Mdenmark huyo alisema: “Hatukuwa katika ubora wetu.

“Tulianza vizuri kwa dakika 10 au 15, tukiwa na nguvu ya mashabiki nyuma yetu – na walibaki nyuma yetu mchezo mzima – lakini Real walifanikiwa kuzitumia nafasi walizopata.

“Tumeruhusu mabao saba sasa katika michezo miwili, jambo ambalo si la kawaida kwetu.

“Sio tu kuhusu mchezo huu, tulifanya hivyo pia wikendi. Tunapaswa kurekebisha na tunapaswa kuifanya haraka.”


3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!

Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.

Kubeti Poa - Bonasi Kubwa

Jisajili sasa

 

Acha ujumbe