Bryan Gil amejiunga na Tottenham kwa dili ambayo ilikuwa inahusisha mbadilishano wa Erik Lamela kwenda Sevilla.

Bryan ambaye alitumia msimu uliyopita kwa mkopo huko Eibar akitokea Sevilla kwa sasa anaiwakilisha Hispania kwenye michuano ya Tokyo Olympics.
Ripoti zilidai wiki iliyopita kwamba Spurs walikuwa karibu kumsaini mchezaji huyo wa umri wa miaka 20 kwa ada ya Β£21.6m jumlisha Lamela ambaye alijiunga na Premier League akitokea klabu ya Roma mwaka 2013.
Wakati hakuna ada ambayo imethibitishwa mpaka sasa, dili imeshakamilika kilichobaki ni Gil kufanyiwa ukaguzi kama uataratibu wa kimataifa unavyotaka.

Gil ambaye amesaini dili ya miaka mitano ameichezea timu ya wakubwa ya Hispania michezo 29 na kufunga mabao 4 na Lamela amefanikiwa kufunga mabao matatu na asisti moja kwenye michezo 33 kwenye mashindano yote msimu uliyopita.
Lamela amesaini mkataba wa miaka mitatu na Sevilla na tavaa jezi namba 17 kwa kampeni za 2021-22.
Gil anakuwa mchezaji wa pili kusajiliwa na Tottenham chini ya kocha Nuno Espirito Santo baada ya kumsajili mlinda mlango Pierluigi Gollini kwa mkopo kutoka Atalanta.
SHOOT! mchezo unaokupa nafasi ya kupambania ushindi wako mkubwa kwenye kasino ya mtandaoni ya Meridianbet! Usisubiri hii, jiunge sasa kufurahia ushindi!




Angelina
Nice update