Fahamu Kuhusu Kai Havertz.

Kai Havertz ametua Stamford Bridge akitokea klabu ya Bayer Leverkusen, ikiwa Lampard anaendelea kukiimarisha kikosi cha Chelsea kwaajili ya msimu mpya.

Harvetz anatarajiwa kuwasumbua mabeki wa timu pinzani pale atakapo ungana na mtaifa mwenzake Timo Werner pamoja na Hakim Ziyech raia wa Morocco.

The Blues wametumia kiasi kikubwa cha fedha katika dirisha hili la usajili, kwa kufanikiwa kumnasa Havertz mwenye umri wa miaka 21 kwa dau linalo ripotiwa kufikia £71m.

Na Havertz hataki kusubiri sana kwani yupo tayari kuleta changamoto mpya baada ya kukamilisha uhamisho wake mapema mwezi huu, alisema: “Nataka kufanikisha mengi yanayowezekana.

Kai Havertz

“Nipo katika taifa jipya, tamaduni mpya najua itanipa shida wiki mbili tatu lakini baada ya hapo nataka kucheza na kufurahia nikiwa na vijana wenzangu.

“Chelsea ni klabu kubwa nataka tushinde mataji, nitajitahidi kucheza kadri ya uwezo wangu naimani tutafanikisha kushinda makombe.

Wakati ada ya uhamisho wa Havertz ikiwa ndiyo yenye kiwango kikubwa katika klabu ya Chelsea lakini kuna ushahidi kwamba Kai alistahili kuuzwa kwa thamani hiyo kutokana na umahiri wake.

Kai Havertz anarekodi ya kufunga magoli 38 na asisti 16 kwenye mashindano yote kwa misimu miwili iliyopita.

Labda swali la kujiuliza, je? ni nafasi ipi itamfaa Havertz katika mfumo wa Lampard.

Werner anatarijiwa kuongoza safu ya ushambuliaji wakati Ziyech na Christian Pulisic watakuwa wakitumika pembeni.Hii inamaanisha Havertz ataliendesha dimba la kati.

Wakati wake Lampard alipokuwa mchezaji aliisaidia chelsea kutwa mataji mbalimbali na kuwa na rekodi ya ufungaji bora alipokuwa akicheza nafasi ya kiungo na Havertz anataka kufuata nyayo za Lampard.

Kuhusu Kai Havertz

Umri: 21

Utaifa: German (Michezo 7, goli 1)

Nafasi: Kiungo Mshambuliaji

Timu ya zamani: Bayer Leverkusen (Michezo 150, magoli 46)

Timu ya sasa: Chelsea

Ada ya uhamisho: £71m


SHINDA NA HI LO

Sasa hii ni rahisi zaidi kupata USHINDI! Unatabiri karata ipi ipo chini au juu, kisha unakusanya mkwanja wako.

Cheza sasa

39 Komentara

    havertz yupo vizuri sana tena sana anajituma

    Jibu

    Asante kwa kutujuza

    Jibu

    Kijana havertz Yuko vizuri@meridianbettz

    Jibu

    asante kwa habar

    Jibu

    Mwalimu Frank lampard atajua namna ya kumtumia na ndo maana kafanikisha kandarasi yake.

    Jibu

    Yupo vizuri

    Jibu

    Takwimu zake zipo vzr sana swal je darajan anawez kutu offer Kama alivyokuwah luverksen ngoj tuone ligi ianze

    Jibu

    Asante kwa makala

    Jibu

    yuko njema sana kjjana

    Jibu

    habari njema

    Jibu

    asante kwa taarifa

    Jibu

    Axante kunijuza hili

    Jibu

    Kijana yupo vizuri

    Jibu

    Havertz kiungo ambae anajua kufunga

    Jibu

    Kai Havertz ndani ya Chelsea anaongeza ugumu kwa Lampard namna ya kupanga kikosi#meridianbettz

    Jibu

    Asante kwa taharifa

    Jibu

    Havertz ni kijana anayejua mpira

    Jibu

    havertz yupo vizuri sana#meridianbettz

    Jibu

    Fundi wa mpila

    Jibu

    Asanteni kwa taarifa

    Jibu

    Lampard hanakazi ya ziada kupanga kikosi chake ukiangalia amesajiri wachezaji mairi wengi wenye kujituma

    Jibu

    Fundi wa mpira

    Jibu

    Kai yupo vizuri katika soka

    Jibu

    Dogo yuko vzur sana bonge la bek

    Jibu

    Yupo vzr

    Jibu

    Lampard Hana haja ya kupanga kikosi aamini ya kwamba amesajili majembe wanaojituma na wenye jitihada, hongera Sana harvetz gud player.

    Jibu

    Havertz Ni talent player

    Jibu

    Kijana anajituma sana.

    Jibu

    Mpambanaji huyo,anajua anachokifanya awapo kiwanjani,noma sana!!!

    Jibu

    Havertz ni moto wa kuotea mbali, Nasubiri kuona maajabu yake ndani ya Chelsea

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Safii

    Jibu

    Lampard anataka kombe msimu huu usajir wake sio mchezo

    Jibu

    Yuko vizuri

    Jibu

    Nazi kwake kocha kupanga kikosi

    Jibu

    Yupo vzr

    Jibu

    Bonge la mchezaji

    Jibu

    Mwalimu Frank lampard atajua namna ya kumtumia na ndo maana kafanikisha kandarasi yake.

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.