Bondia Gennady Golovkin alimpiga kwa Knock Out bondia wa kijapani Ryota Muarata siku ya Jumamosi na kuongeza mkanda wa WBA na sasa amefuzu kuchapana na Saul ‘Canelo’ Alvarez katika pambano lao la mara ya tatu.

Golovkin Amkarisha Murata kwa KO Raundi ya 9

GGG ambaye alifikisha miaka 40 siku ya Ijumaa alimpiga Murata katika raundi ya 9 ya pambano huko Saitama, kaskazini mwa Tokyo baada ya kutopigana kwa miezi 16 na kuongeza idadi ya KO zake kufika 37.

Murata alionekana kuwa imara katika raundi za awali kwa kupiga makonde kadhaa ya mwili Golovkin na GGG alionekana kuwa kwenye wakati mgumu kabla ya kuusoma mchezo na kutawala katika raundi ya sita mpaka alipomuangusha Murata katika raundi ya tisa.

Golovkin sasa ataelekeza mawazo yake kwenye uwezekano wa kupata pambano la tatu dhidi ya mfalme wa pauni kwa pauni, Alvarez katika pambano la trilogy baadaye mwaka huu, baada ya kumsukuma Mexiko huyo katika pambano mbili za awali.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa