Baada ya mechi kibao kuchezwa wikendi iliyopita leo ni zamu ya Crystal Palace dhidi ya Arsenal ndani ya dimba la Selhurst Park mchezo wa Premier League.
Ni vita ya makocha wawili ambao waliwahi kuichezea Arsenal hapo nyuma katika eneo la kiungo Patrick Viera kocha wa Palace akimkaribisha Mikel Arteta. Kikosi cha Arteta kina kumbukumbu ya kuidungua 1-0 Aston Villa kabla ya mapumziko ya kimataifa wakati Palace ilienda sare ya bila kufungana na Man City.
Taarifa ya Timu
Crystal Palace wanaweza kuwakosa Michael Olise na Wilfried Zaha, ambao wamekuwa wakiuguza majeraha ya mguu na nyama za paja.
The Eagles pia wanaangalia uzima wa James McArthur na Nathan Ferguson.
Mlinda mlango wa Arsenal Aaron Ramsdale anatazamiwa kukosa mechi ya pili kutokana na jeraha la misuli.
Bukayo Saka amerejea mazoezini baada ya kujiondoa kuichezea timu ya taifa ya England kutokana na ugonjwa na anatarajiwa kucheza leo.
Takehiro Tomiyasu, ambaye hajashiriki kwa wiki 10 kwa sababu ya tatizo la majeraha, amerejea mchezoni.
3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.