Siku ya leo Alhamisi kulizuka uvumi kwamba wachezaji wa Manchester United kuwa kwenye vita kali ya kugombea unahodha wachezaji hao ni Harry Maguire na mshambuliaji nyota Christiano Ronaldo.

Maguire Avunja Ukimya Juu ya Uvumi wa Kugombea Unahodha

Sasa Maguire amekanusha madai ya vita kati yake na Cristiano Ronaldo katika chumba cha kubadilishia nguo kuhusu unahodha wa klabu hiyo. Harry Maguire amekanusha vikali ripoti za “vita vya nguvu” na Cristiano Ronaldo kuhusu nafasi ya unahodha wa Manchester United.

Ripoti zinadai kwamba Ronaldo anataka kuwa nahodha wa kudumu wa Manchester United na tayari kumekuwa na maneno kutoka kwa mashabiki wa klabu hiyo kutaka cheo hicho apatiwe Ronaldo ingawa kuna baadhi wanataka Maguire aendelee kwenye nafasi yake.

Maguire aliandika kwenye akaunti ya Twitter: “Nimeona ripoti nyingi kuhusu klabu hii ambazo si za kweli na hii ni nyingine. Sitaanza kutuma juu ya kila kitu kilichoandikwa lakini nilihitaji kuweka hii wazi. Sisi ni United na tunazingatia zaidi mchezo wa Jumapili. Furahia siku yako kila mtu.”


KASINO YA MTANDAONI: EMOTICOINS SABABU YA KUVUNA ZAIDI.

Haijawahi kuwa rahisi hivi kwenye safari yako ya kuvuna mkwanja, kasino maridhawa ya meridianbettz inakuletea mchezo wa Emoticoins unaokupa nafasi ya kufanya safari yako kuwa rahisi zaidi. Wakati ni wako nafasi ni yako na Emoticoins.

senegal, Senegal Mabingwa AFCON 2021., Meridianbet

CHEZA HAPA.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa