Michuano ya kombe la Dunia mwaka 2022 inatarajiwa kuanza kurindima mwezi Novemba na kuhitimishwa Desemba huku Qatar ambayo ndiyo nchi ndogo zaidi akiwa ndiyo mwenyeji wa mashindano hayo.
Qatar baada ya kuchaguliwa kuwa mwenyeji wa Kombe la Dunia mwaka 2010 walianza kuboresha viwanja na kujenga vingine vipya ambapo pia katika harakati za ujenzi wa viwanja hivyo kuliingia dosari kwa kulalamikiwa na baadhi ya watu kufuatia unyanyasaji wa wafanyakazi zaidi ya milioni 2 ambao ni wageni huku ikiripotiwa maelefu ya wafanyakazi walifariki wakati wa ujenzi.
Waandaaji wanasema viwanja vyote vilijengwa kwa kuzingatia kanuni za mazingira, huku vyote vikipata nyota nne au tano kutoka kwa Mfumo wa Tathmini Endelevu Duniani (GSAS). Bajeti ya awali ya kujenga viwanja na maeneo ya mazoezi ilikuwa £4.7bn.
Hivi ni viwanja 8 vitakavyotumika kuchezwa kwa Kombe la Dunia 2022 la Qatar
Lusail Stadium (2022)
Uwezo kubeba mashabiki: 80,000
Michezo: 10 pamoja na Fainali
Mahali: Lusail
Al Bayt Stadium (2021)
Uwezo kubeba mashabiki: 60,000
Michezo: 8 pamoja na mchezo wa ufunguzi
Mahali: Al Khor
Stadium 974 (2021)
Uwezo kubeba mashabiki: 40,000
Michezo: 7 mpaka hatua ya 16 bora
Mahali: Doha
Khalifa International Stadium (1976)
Uwezo kubeba mashabiki: 45,416
Michezo: 8 pamoja na mshindi wa tatu
Mahali: Doha
Education City Stadium (2020)
Uwezo kubeba mashabiki: 40,000
Michezo: 8 Mpaka robo fainali
Mahali: Al Rayyan
Al Thumama Stadium (2021)
Uwezo kubeba mashabiki: 40,000
Michezo: 8 Mpaka robo fainali
Mahali: km 12 kusini mwa Doha
Muundo kama kofia ya kiarabu/ barakashia
Al Janoub Stadium (2019)
Uwezo kubeba mashabiki: 40,000
Michezo: 7 mpaka hatua ya 16 bora
Mahali: Al Wakrah
Ahmad Bin Ali Stadium
Uwezo kubeba mashabiki: 40,000
Michezo: 7 mpaka hatua ya 16 bora
Mahali: Al Rayyan
3500 NI YAKO UKIJIUNGA TU MERIDIANBET!
Una nafasi ya kupata bonasi ya shilingi 3500 kwa ajili ya kuanza safari yako ya kasino ya mtandaoni ya Meridianbet.