Bondia Dillian Whyte ameitaka mechi ya marudiano na Tyson Fury baada ya kupoteza kwa TKO katika raundi ya sita siku ya Jumamosi katika uwanja wa Wembley ambapo mashabiki 94,000 wa mchezo huo walishuhudia pambano hilo.

Whyte Anataka Mechi ya Marudiano na Fury

Fury ambaye alitetea mkanda wa WBC aliendeleza rekodi yake ya kutopoteza katika mapambano yote aliyocheza na alitangaza kwamba baada ya pambano hilo atastaafu mchezo wa masumbwi.

Lakini Whyte amelalamika kwamba hakutendewa haki na mwamuzi wa pambano hilo kwani alipaswa kupewa muda wa kurejea katika utimamu ilikuendelea na mchezo lakini mwamuzi alikatisha na angependa mechi ya kurudiana licha ya Gypsy King kutangaza kustaafu.

Aliiambia Sky Sports: “Nilipigwa sehemu mbaya lakini ni wazi nilikuwa najaribu kurejesha fahamu zangu na alinisukuma na nikaanguka na kugonga kichwa changu kwenye turubai, jambo ambalo ni kinyume cha sheria.

“Huu sio mchezo wa mieleka, huu ni mchezo wa ngumi, nilipaswa kuongezewa muda wa kukaa sawa kisha niendelee na pambano.

“Alisema atastaafu. Natumai hatastaafu kwa sababu nataka pambano la kurudiana tena.


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa