Barcelona imekuwa na wakati mzuri kwenye dirisha ka usajiri majira haya ya kiangazi ambapo wamefanikiwa kusajiri majina makubwa kama Robert Lewandowski, Raphinha, Franck Kessie na Andreas Christensen mpaka sasa.

Wakati wakiendelea na kufanya sajiri bado, wana mtihani wa kufanikisha kuweza kuwaingiza wachezaji wote waliosajiri kwenye klabu hiyo ili waweze kuingizwa kwenye payroll ya klabu, hapo ndipo changamoto ilipo kutokana na sheria za fedha za La Liga.

Barcelona, Barcelona na Kisanga cha Wachezaji Wapya Kusajiriwa kikosini, Meridianbet

Raisi wa La Liga Javier Tebas, wakati akihojiwa kwenye kipindi cha La Liga “Kick Off” Gala kuhusu hali ya sasa ya klabu ya Barcelona kuweza kuwasajiri wachezaji hao kwenye payroll ya klabu hiyo alijibu.

“Barcelona wapo kwenye njia sahihi ya kuwasajiri, bado kuna taarifa za kukamilisha, lakini wana muda.” Alisema raisi wa La Liga Javier Tebas.

Alipoulizwa zaidi kuhusu Barcelona wanaweza kuwatumia wachezaji wapya kwenye siku ya kwanza ligi itapoanza, Tebas alijibu, waulizwe FC Barcelona. Ninachoweza kusema kwamba wanajua kanuni vizuri na wanajua nini wanapaswa kufanya. Wanapaswa kufanya hivyo, lakini bado wana muda.

“Wameuza hati miliki ya matangzo ya TV kwa €207 million. Kisha wameongeza hisa 25% ambapo nadhani itwapatia €350 million zaidi au inaweza fika €500 million na nafikili kuna mauzo mengine, mpango wa tatu unaweza wapatia  takribani €200 million.

“Pia, ikiwa watafanikiwa kuuza baadhi ya wachezaji, hii inaweza kuwapa nafasi ya kuwasijiri hawa. Wamefanikiwa kuuza dhamana zao, kitu ambacho walipaswa kufanya, na kupunguza mishahara, hilo ndilo litakalowapa nafasi ya kusajiri.”

 

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa