Pogba Kukosekana Kombe la Dunia Qatar 2022

Nyota wa klabu ya Juventus na mchezaji wa kimataifa Paul Pogba anweza kukosa michezo yote ya kombe la dunia nchini Qatar kutoka na kupata majeraha ya goti ambayo anapaswa kufanyiwa upasuaji.

Pogba anatarajia kukutana na mtaalamu kwa ajiri ya ushauri wa tiba gani itamfaa, kwani mpaka sasa tayari keshafanyiwa vipimo vya kuangaliwa jeraha la goti lake la kulia baada ya kuondoka mazoezini jijini Los Angeles wiki iliyopita.

Mchezaji huyo wa kimataifa wa Ufaransa mwenye miaka 29, alitarajiwa kufanyiwa upasuaji nchini Marekani bila ya kusafiri na timu ambayo inaendelea na safari ya michezo ya Pre-Season.

Pogba ananjia mbili za tu za kufanyiwa upasuaji ambapo moja ni kuondoa kipande “meniscus”  ambapo upasuaji wake utamuweka nje kwa siku 40 hadi 60, lakini oparesheni hii inawafaa zaidi vijana.

Opareshani wa pili kuziba sehemu yanye shida, lakini itambidi akae nje kwa muda wa miezi minne hadi mitano, na michezo ya kombe la dunia inatarajiwa kufanyika mwezi wa Novemba na December inamaana hata weza jumuishwa kwenye kikosi cha timu hiyo.

 

Acha ujumbe