Kocha wa klabu ya Simba SC Zoran Maki ameweka wazi sababu ya kupoteza mchezo wake wa kirafiki dhidi ya klabu ya Haras El Hodoud  kwa goli 2-0 kwenye dimba la Haras El Hodoud nchini Misri.

Kikosi cha Zoran Maki mpaka sasa kikiwa nchini misri mchezo dhidi ya Haras El Hodoud ni watatu tangu waweke kambi nchni humo huku wakiwa wamepoteza michezo miwili ambayo ni dhidi Haras El Hodoud (2-0) na Al Akhdood (6-0) na wakipata sare na Ismaily (1-1)

zoran, Zoran: Simba Haikuwa Bora Kwenye Kiungo na Uwanja Mbovu, Meridianbet

“Hatukuwa bora kwenye eneo la kati, hatukutengeneza nafasi nyingi, nafasi moja pekee. kiwanja hakikuwa kwenye hali nzuru lakini hili sio sababu, hatukutengeneza nafasi, haukuwa mchezo mzuri.” Alisema kocha wa simba Zoran Maki  baada ya mchezo kuisha

Simba iliondoka nchini Julai 14 mwaka huu, kuelekea kwenye mji wa Ismailia nchini Misri kwa ajili ya kuweka kambi na kujiandaa na michezo ya msimu ujao wa 2022/23.

Simba na Yanga wanatarajia kukutana kwenye Ngao ya Jamii itakayopigwa Agosti 13, kwa ajiri ya ufunguzi wa ligi msimu huu, baada ya Yanga kufanikiwa kuchukua makombe yote msimu Uliopita na sheria za ligi zinampa nafasi aliyeshika nafasi ya pili kucheza mchezo wa ngao ya jamii.

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa