Benzema Nje Mechi Dhidi ya Villarreal.

Karim Benzema ataukosa mchezo wa Real Madrid katika LaLiga dhidi ya Villarreal siku ya Jumamosi baada ya kutokuwa sawa kutokana na jeraha alililopata wakati wa mchezo dhidi ya Valencia.

Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 32 alitolewa dakika ya 76 ya mchezo kwenye mchezo ambao Real Madrid ilipokea kipigo cha 4-1 katika dimba la Mestalla .

Benzema Nje Mechi Dhidi ya Villarreal.
Karim Benzema

Lakini alianza kufanya mazoezi na ilikuwa ni ishara huenda akarejea lakini pia huenda Zinedine Zidane ameweka jicho lake kwenye mchezo wa Champions League dhidi ya Inter siku ya Jumatano kwa kutotaja jina lake kwenye mchezo wa wikendi hii.

Benzema ndiyo kinara wa upachikaji mabao kwa timu ya Real Madrid msimu huu akiwa ameweka kambani mara nne katika michezo nane aliyocheza, lakini pia ametoa asisti tatu kuliko mchezaji yoyote wa Los Blancos akiwa sambamba na Rodrygo.

Luka Jovic pia ataukosa mchezo huo baada ya kukutwa na virusi vya corona siku ya Ijumaa wakati pia Casemiro na Eder Militao ambao walikuwa wamejitenga kufuatia kuwa na COVID-19 kabla ya mechi za kimataifa nao pia wapo nje ya kikosi.

Sergio Ramos alipata maumivu ya nyama za paja wakati wa mchezo wa kimataifa Spain dhid ya Ujerumani na Spain ilishinda kwa 6-0 nahodha huyo anatarajia kuwa nje ya dimba kwa muda wa siku 10 hii inamaanisha ataukosa mchezo wa Jumamosi.

Zidane alisema: “Tunachotakiwa kufanya ni kuweka makundi,” unaongelea mchezo wa jumamosi na Jumatano ni muhimu zaidi kwenye mchezo wa Champions League lakini mechi zote ni muhimu.

Madrid wapo nafasi ya nne kwenye msimamo wa LaLiga alama nne nyuma ya vinara wa ligi hiyo Real Sociedad ambao wamecheza mechi nyingi.


BASHIRI UKIWA MAHALI POPOTE!

Hauhitaji kuwaza linapokuja suala la ubashiri na odds kubwa. Bashiri na Meridianbet ukiwa popote ufurahie ushindi mkubwa katika michezo mbalimbali na hadi milioni 16 kwenye michezo ya kasino.

Meridianbet Beti Popote

INGIA MCHEZONI!

18 Komentara

    Pole sana Benzema

    Jibu

    pole sana kwake atakuwa tu sawa

    Jibu

    Get well soon Benzema

    Jibu

    Daa pole Sana benzema

    Jibu

    Hii habari mbaya kwa mashabiki wa Real madrid

    Jibu

    Pole Sana

    Jibu

    Pole Sana Benzema

    Jibu

    Get well soon

    Jibu

    Mungu akupganie ukae sawa

    Jibu

    Pole sana kwake

    Jibu

    Pole sana

    Jibu

    Pole sana

    Jibu

    pole sana

    Jibu

    Pole sana soon atakuwa sawa

    Jibu

    Pole Benzema

    Jibu

    Pole sana

    Jibu

    pole yake

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.