Chama Cha Soka Nchini Ghana Kitaendelea Kusimamisha Ligi Yake

Chama cha Soka nchini Ghana (GFA) kimetangaza kuwa msimu wa mpira wa miguu wa 2019/20 unasalia kusimama kwa sababu ya janga la COVID-19..Msimu huo, umeahirishwa tangu Machi 16, 2020, hadi hapo ilani zaidi baada ya marufuku ya serikali dhidi ya mikusanyiko yote ya umma.

Halmashauri Kuu katika mkutano wake iliamua kwamba hali hiyo inabaki, ikisisitiza kwamba Chama hicho kiko katika mashirikiano kadhaa na Serikali, Wizara ya Afya, Huduma ya Afya ya Ghana, Wizara ya Vijana na Michezo, GFA Kamati ya Matibabu, CAF na FIFA…. Halmashauri Kuu iliamua zaidi kuwa Chama kitaendelea kufuatilia hali hiyo na wataitazama tena Juni 30, 2020 baada ya kukagua kwa uangalifu na tathmini ya suala hilo na kuchukua maamuzi mengine zaidi.

Wakati huo huo Taarifa ya GFA inasema, itazingatia mambo yote wakati huo na itachukua maamuzi yote muhimu ili kuhakikisha usalama wa washiriki wote na kukamilika kwa msimu vizuri. Ghana mpaka hivi sasa ni miongoni mwa Nchi chache Afrika zilizopanga msimu wa mpira wa miguu Kuendelea kuchezwa.

5 Komentara

    Afya ni bora na chaguo la kwanza kama hali bado wasubili tu

    Jibu

    Hli ni jambo la msingi sana. Pongezi kwa Chama cha Soka nchini Ghana (GFA)

    Jibu

    Uwamuzi nzuri

    Jibu

    Ni Jambo la msingi

    Jibu

    Ni vyema sana kwa timu hii

    Jibu

Acha ujumbe