Kingsley Coman amesema atawashauri wachezaji wenzake wa Bayern Munich namna ya kumzuia nyota wa Paris Saint-Germain Kylian Mbappe siku ya fainali ya Champions League.
Mbappe alikuwa akisumbuliwa na jeraha la kifundo cha mguu alililopata katika fainali ya Coupe de France dhidi ya Saint-Etienne lakini kwa sasa anaonekana yupo fit kuwakabili wababe wa Ujerumani Bayern Munich.
Mchezaji huyo mwenye umri wa miaka 21 mchezaji mwenzake na Coman katika timu ya taifa ya Ufaransa aliiokoa PSG dakika za majaeruhi dhidi ya Atalanta akitokea benchi na kuchangia katika magoli yaliyoipa ushindi na kufuzu kucheza nusu fainali iliyowakutanisha na RB Leipzig siku ya Jumanne na PSG ilipata ushindi wa 3-0 na kuwaondosha Leipzig.

Bayern walimzuia Lionel Messi kwenye mchezo wa robo fainali ambao uliwakutanisha Bayern Munich na FC Barcelona mchezo uliyomalizika kwa Barcelona kula kichapo cha historia 8-2 na Coman amepanga kusaidia timu yake katika kumkabili Mbappe asilete madhara katika dimba la Estadio da Luz siku ya Jumapili.
“Nimecheza naye mara kadhaa, kwa hiyo nitajaribu kutoa ushauri kwa wachezaji wenzangu namna ya kumdhibiti,” Coman alikuwa akimuongelea Mbappe.
“Pia kuna video na maelekezo ya mwalimu .katika hili, tutajaribu kumzuia ni mshambuliaji ambaye analeta madhara kama ukimruhusu kuipita safu ya ulinzi,kama tulivyo mchezea messi tunapaswa kumzuia na Mbappe.
Wakati Mbappe alikuwa sehemu ya timu ya taifa ya Ufaransa iliyo shinda kombe la dunia mwaka 2018 nchini Urusi, Coman hakuwepo katika kikosi kutokana na majeraha.
Winga huyo wa Bayern amesema hiyo ilisha pita na haiwezi kuleta hamasa yoyote kufikia mafaniko katika Champions League.
“Bado ningependa kushinda kombe la dunia lakini kwa sasa nipo na klabu yangu nataka kushinda Champions League na natumaini tuta beba taji siku ya Jumapili.” alisema Coman.
Drops and Wins!
Umeijua hii? Ni promosheni kabambe ya ushindi kwenye Casino ya mtandaoni ya Meridianbet! Unaweza kushinda hadi Euro 2,000,000 leo.


Caroline
Sidhani Kama utaweza kumdhibiti.Mbapee ni level nyingine
Ester jackson
Bayern kweli wamejipanga dhidi ya mashambulizi kwa PSG haswa wakiangalia ambao wako vizuri kwenye timu pinzani na tukiangalia vizuri kuwa mbappe yuko vizuri sana lakini sio kiafya zaidi mana hajakaa mda mrefu kwenye matibabu yake neymaar hatujajua kama atashiriki kwenye mchezo au laah hivyo PSG wananafasi ndogo sana kushinda kwenye mchezo huo.
warda
Daaaa!!! jamani wesha anza kuwaundia zengwe #Meridianbettz
Mwajumah
Wataweza kweli kumdhibit mbappe maana ni Moto wa kuotea mbali#Meridianbettz
rama
Maoni:wasije wakajisahau kuwa kuna mchezaji atari zaid neymar
felister
hahaha aangalie tu wasije wakadhibitiwa wao
Zeiyana
Bayern much vs PSG hili gemu litakua si la mchezo ukiangalia mbappe ndoto yake yote kuipelekea timu yake kuchukua ushindi
Shan
Kila kitu kinawezekana juhudi tu!
Dorophina
Bayern hawawezi kumdhibiti mbappe dogo kiwango kingine
Adelta
Asante kwa taarifa @meridianbettz
Khadija
kila kitu kinawezekana juhudi tu#meridianbettz
Magdalena
bayern wajitume sana katika kunyakua kombe nafasi wanayo nzuri tu
Fatina mfingi
Hakuna kinacho shindikan chin ya jua kikubwa Iman na kijituma tyuuuuu
JULIANA
Wananzengo awakosekani
Lydia Emmanuel Magoti
Watanzaje kumzibiti mbappee kwamfano mbappee akiwa uwanjani akoseagi kitu wafanye kaz kweli hapo
Samira
Mbappe ni moto wa kuotea mbali wasijipe moyo hivyo waandae mbinu za kumkabili
Tatu
Mbappe ni mchezaji mahili pia timu ya PSG imejipanga kisawasawa
Janeflora malisa
Jitaid kwa hilo
Sadick
Tangu apate majeraha Mbappe hajacheza kwa kiwango chake nadhani haitakuwa kazi kubwa kwa Bayern kumuzuia#meridianbettz
Sabrina
Kylian Mbappe yuko vizuri coman na wenzie wajipange ile ile.
Hope mwaikuka
Sina uhakika na hilo
Samiah
Sina uhakika nahilo
Furahav
Watafanya jambo la mana kumkaba mbappe,mana wakizubaa tu wamekisha.
Gabriel
PSG wajipange maaana Bayern Munich sio watu wazur wako vzur sana na wamejipanga kila upande
Issa
Koman unakosea psg sio mbape utafeli vibaya final hii
Devotha
Bayern wako vizuri pia PSG wapo vizuri sijui karata yangu niitupe wapi! Nikiangalia safu ya ushambuliaji timu zote zipo vizuri Ila kwenye safu ya ulinzi mmmh! Lakini historia inasema walishakutana mara nane na PSG wameshinda mara tano uku Bayern wakishinda mara tatu. Ngoja tuone je wataweza kumdhibiti Mbappe?
Shafii
Dk90 zitaongea.
Omary lukumbi
Kudefence must be him
Sauda
Mbappe hawezi kudhibitiwa kirahisi hivyo
aisha
Ngoja tuone matokeo
Povel
Mpr dk 90 ngoj tuone
farida ahmadi
Maneno tyuu hayo ngoja tujionee wenyewe mashabiki