Djuma Shabani , Huduma Yake Dimbani ni Zaidi ya Kujituma

Djuma Shabani ni moja ya Mabeki wa pembeni wanaotisha katika ligi yetu msimu huu kutokana na kiwango Cha kuvutia ndani ya kiwanja akiwa mwiba kwa safu ya ulinzi ya timu pinzani kutokana na uwezo wake mkubwa wa kutengeneza nafasi za mabao na kuisaidia Klabu yake ya Yanga.

Siku zote Djuma Shabani akivuka mstari wa katikati ya Kiwanja hugeuka kuwa kama kiungo mshambuliaji mikimbio yake kuelekea katika eneo la wapinzani wake huwa na faida kubwa kwa timu yake ndiyo maana mara nyingi kwa sasa mabao ya Yanga hutengenezwa kutoka upande wa kulia eneo ambalo Djuma Shabani husimama.

djuma shabani
djuma shabani

Djuma Shabani huyu ni mwalimu wa kupiga krosi sahihi katika box la wapinzani kwa upande wa Mabeki wa pembeni katika ligi yetu kwa sababu ana uwezo wa kupiga Mpira mrefu na ukafika eneo sahihi mfungaji akatupia (hapa Mayele kafaidika zaidi) pia ana uwezo wa kupiga krosi za chini nazo zikawa na faida kwa timu yake tofauti na Mabeki wengine wa pembeni ambao mara nyingi Mipira yao huishia kwa Mabeki wa timu pinzani hivyo katika eneo hili Djuma ni mwalimu wao hakuna kama yeye.

Mfalme wa zamani wa kabila la Hun (Attila the Hun) aliwahi kusema siyo vibaya kujifunza kwa aliye kuzidi hivyo ni wajibu wa Mabeki wa pembeni kujifunza kutoka kwa Djuma Shabani kama wakiweza kucheza kama anavyo cheza mwamba huyu itakuwa na faida kubwa kwa Vilabu vyao na Taifa letu.

Katika ulimwengu soka hivi sasa Mabeki wengi wa pembeni hutumika kutengeneza nafasi za kufunga huku mawinga wakigeuka kuwa wafungaji zaidi hivyo Djuma Shabani anatupa somo unaweza kuwa mlinzi wa pembeni na ukawa kinara wa Assist kama ambavyo yeye ameshafanya akiwa katika ligi ya DR Congo.

Imeandikwa na Emanuel Mwayombo.


VUNA MKWANJA NA AVIATOR

Maana halisi ya ushindi mkubwa unaipata katika kasino ya mtandaoni ya Aviator kutoka meridianbettz. Andaa kapu la ushindi wa mkwanja na beti kibao za BUREEE.

 

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

SOMA ZAIDI

Acha ujumbe