Manchester United itawabidi wasubiri mpaka makocha Jurgen Klopp na Pep Guardiola wa Manchester City na Liverpool waondoke ili waweze kushinda tena taji la Premier League,hii ni kwa mujibu wa Gary Neville.

Man United wanaukame wa kombe la Premier League tangu Sir Alex Ferguson alipofanya hivyo mwaka 2012-13 na wamefanikiwa kufika nafasi ya pili mara moja pekee.

Licha ya kufanya vyema katika mzunguko wa pili wa msimu uliyopita wa ligi kuu ya Uingereza, timu hiyo iliyo chini ya kocha Ole Gunnar Solskjaer ilimaliza nafasi ya tatu alama 33 nyuma ya mabingwa wa EPL 2019-20, Liverpool ambao pia walimaliza ukame uliyo dumu miaka 30 na point 15 nyuma ya Man City ambao walinyang’anywa ubingwa huo na Liverpool.

Man United Watashinda EPL Klopp na Guardiola Wasepe.
Klopp na Guardiola

Klopp alimaliza ukame wa miaka 30 ya kusubiri kunyanyua kombe hilo na tayari Liverpool wameuanza msimu mpya vizuri kwa kuwafunga Leeds waliyopanda daraja msimu huu goli 4-3.

         Anacho kiamini Gary Neville Kuhusu Man United Kushinda EPL tena.

Beki wa zamani wa upande wa Kulia wa United Neville amesema kwa kujiamini kwamba Manchester United wataongeza rekodi ya 21 ya kutwaa taji la Premier League lakini watafanya hivyo kama Makocha wa Anfield na Etihad Stadium wakiondoka.

“Kitu Kimoja nakuhakikishia Man United watashinda tena,” aliiambia The Mirror.

“Hilo linaweza lisitokee mwaka huu wala mwaka ujao, lakini itaku vizuri sana kama wakishinda tena EPL, na hakika hata Chelsea wanafikiria kama ninavyo fikiria itachukua muda kidogo kumaliza utawala wa Guardiola na Klopp.

Man United Watashinda EPL Klopp na Guardiola Wakisepa.

Man United wamekuwa katika tetesi kubwa za kumsaini kiungo wa Borussia Dortmund Jadon Sancho katika madirisha yote ya usajili lakini Neville ameshauri kama Man United wana nia ya kushinda ubingwa wanahitaji kufanya usajili wa wachezaji wengi.


SHINDA NA MERIDIANBET!

Tengeneza pesa kidijitali kwa kubashiri mbio za farasi hapa Meridianbet! Chagua nani ashinde, unakusanya mkwanja.

Cheza Sasa.

42 MAONI

  1. Naamini man u msimu huu watajipanga vizuri sana kuucheza vizuri msimu huu wa Epl wanaweza wakabeba kombe cha msingi ni kujipanga vizuri

  2. Hilo linaweza lisitokee mwaka huu wala mwaka ujao, lakini itaku vizuri sana kama wakishinda tena EPL, na hakika hata Chelsea wanafikiria kama ninavyo fikiria itachukua muda kidogo kumaliza utawala wa Guardiola na Klopp.#meridian

  3. Kwa upinzani unajionyesha Uingereza sidhani kama Pep na Klopp wanaweza kutawala miaka nenda miaka rudi bila kutokuwa na mapinduzi ndani ya Uingereza, Ni wakati ambao machopa wachanga na Chipukizi watakuja kufanya mapinduzi makubwa sana ndani ya EPL

  4. Maoni yake mkongwe neville natumain Kama watecheza kwa kujitumah wachezaj na club kufany usajil sehem zenye mapunguf natumain Taj wanawez chukuwah la Epl

  5. Naamini man u msimu huu watajipanga vizuri sana kuucheza vizuri msimu huu wa Epl wanaweza wakabeba kombe cha msingi ni kujipanga vizuri

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa