Klabu ya Barcelona imethibitisha kumpa kazi ya ukocha wa timu yao ya vijana (Barcelona B) Rafael Marquez ambaye aliwahi kuichezea klabu hiyo.

Rais wa Barca Joan Laporta alibainisha mapema mwezi huu kwamba mazungumzo ya kumrejesha Marquez kama kocha wa vijana na siku ya Alhamisi ilithibitishwa rasmi.

Mchezaji huyo wa zamani wa Mexico aliwakilisha mara tano taifa kwenye michaunao ya kombe la Dunia na sasa anaenda kufuata nyayo za Pep Guardiola na Luis Enrique katika kuisimamia Barcelona B.

Marquez amesaini mkataba wa miaka miwili ambao utaisha 2024 na siku ya Ijumaa ataanza rasmi kufanya kazi pia ukurasa rasmi wa Twitter wa klabu hiyo ya Laliga uliandika: “Karibu tena nyumbani Rafa”


CHEZA KASINO HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa