Oblak - Tutajua Baada ya UEFA Kufika Mwisho.

Golikipa wa Atletico Madrid Oblak amesema kwamba hatima yake katika timu ya Atletico itajulikana baada ya Champions League kumalizika. Golikipa huyo wa Slovenia amekuwa akihusishwa kuuzwa Chelsea baada ya kudumu Atletico Madrid kwa Misimu sita.

Kuelekea mchezo wa robo fainali kwenye michuano ya Champions League ambapo Atletico ataumana na RB Leipzig siku ya Alhamisi, Oblak amesema kwa sasa anaangalia mchezo huo wa robo fainali ikiwa Atletico madrid wanajaribu kuwinda taji la mabingwa wa ulaya kwa mara ya kwanza.

Kushinda kombe la Europa League miaka miwili iliyopita kunaipa shauku Atletico kushinda Champions League msimu huu, ikumbukwe Atletico walishafika fainali kwenye mashindano hayo lakini hawakufanikiwa kutwaa taji hilo la hadhi ya juu msimu wa 2015-16 walipokutana na Real Madrid.

“Huu sio muda wa kuongelea hilo, sasa ni Leipzig,” aliiambia AS wakati alipoulizwa kuhusu uvumi unaendelea juu ya yeye kutua Chelsea.

“Tutajua kwenye mchezo wa mwisho kwa sasa kuna michezo mitatu imesalia, baada ya hapo tunaweza kuzungumza, lakini kwa sasa ni Leipzig nataka kweli tupite hatua hii.

“Wote tuliyopo hapa Lisbon tunastahili ushindi, lakini nadhani wakati wetu unakuja. Ni ngumu kufikiria nyuma ya huu mchezo, tunatakiwa tuwapige Leipzig nakisha tuangalie mambo mengine.

“Pia nitafurahi sana, pia hata katika timu kama tukifanikiwa kushinda Champions League.

Wakati Atletico wakiwa wanajiandaa na mchezo huu kuna mapungufu yalijitokeza kwa baadhi ya wachezaji wao wawili kukutwa na virusi vya Corona wachezaji hao ni mshambuliaji Angel Correa na beki Sime Vrsaljko.

Oblak alisema kila mtu alipata wasiwasi baada ya hali hiyo kujitokeza pia aliongeza kwa kusema “ni aibu” kwamba Angel Correa na Sime Vrsaljko watakuwa nyuma ya Madrid.

Golikipa huyo wa Atletico anaweza kufurahia kukosekana kwa mshambuliaji hatari wa Leipzig aliyetimkia Chelsea Timo Werner.

Lakaini Oblak hakutaka kuongea sana badala yake aliwashauri Leipzig kutafuta mbadala wa mshambuliaji wao huyo aliyeihama timu hiyo.


Umekuwa mteja muaminifu wa meridianbet? Kuna zawadi kibao hadi 5% ya pesa yako inarejeshwa kwako. Kila wiki unaweza kurudishiwa mpaka Tsh 250,000.

soma zaidi

44 Komentara

    Sidhani kama Atletico watamuachia kirahisi Oblak

    Jibu

    Safi san hii makala imetulia kiukweli

    Jibu

    oblack angebaki tu atletico

    Jibu

    Naona tayari Chelsea imeshatupa ndowana ni dalili za kutaka kujiunga Stamford Bridge#meridianbettz

    Jibu

    Makala safi sana

    Jibu

    Chelsea hapo ridhani kama watamuacha tunasubiri tu mechi iishe tujue nani ameenda na nani anabaki ili usajili uzidi kuwa mzuri

    Jibu

    Mh hapa kazi ipo

    Jibu

    Oblak kama unaona utapata mafanikio sio mbaya nenda tuu sisi mashabiki kila la kheri

    Jibu

    Duuh kazi ipo

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Ngoja tujihone hapo

    Jibu

    Oblack ni kipa mzuri Sana

    Jibu

    Kikubwa pesa Chelsea inabid wawek dau linalowez kuwashawish Atletico Madrid kumwachia oblak

    Jibu

    Acha tuone mwisho wa uefa

    Jibu

    Maoni:ngoja tuone atletico wata muachia aondoke

    Jibu

    du hapo kazi ipo#meridianbettz

    Jibu

    Makala Safi

    Jibu

    Ngoja tujionee apo#Meridianbettz

    Jibu

    Mhmh ngoja tuone Kama watakubali
    @meridianbettz

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Habari njema

    Jibu

    Asante kwa makala#meridianbettz

    Jibu

    Kazi ipo

    Jibu

    Safi sana

    Jibu

    Oblak n kipa mzur sana hawez kuondoka bila kupatikana mbadala wake

    Jibu

    Atletico hawawezi kumuacha Oblak aende

    Jibu

    Mko vinzur

    Jibu

    Tusubirie hitimisho

    Jibu

    Sahihi

    Jibu

    Soon Italia chombo ya chelsea

    Jibu

    kila kitu mipngo ajipnge

    Jibu

    Mipango muhim

    Jibu

    oblack aende tu chelse akaokoe gurudumu

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Asante kwa taarifa

    Jibu

    Oblack abaki tu atletico

    Jibu

    Maamuz yafanyike!!

    Jibu

    Sa itakuaje

    Jibu

    Sidhani kama Atletico watamuachia kirahisi Oblak kwa maana bado wanamwitaji

    Jibu

    Ila Oblak Amekaa sana Atletico#Meridianbettz

    Jibu

    Oblack karibu Chelsea.

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.