Uongozi wa Klabu ya Azam FC hatimaye imeamua kuwa ya utofauti kwa kutangaza kuwa kuanzia kesho watapocheza na Dodoma Jiji FC, mechi zote za ligi zitakazochezwa Azam Complex mashabiki wataingia bila kutoa kiingilio.

Ibwe alisema wamefikia hatua hiyo ili kuwapa nafasi mashabiki wa timu hiyo kuja kuiyona na kuisapoti timu yao kila itakapokuwa inacheza mchezo wa ligi na kitu pekee ambacho mashabiki wanatakiwa kuwa nacho ni jezi ya Azam FC.

Azam, Kuwaona Azam FC Chamazi ni Bure, Meridianbet

Ibwe alifunguka kuwa: “Mashabiki hawatalipa kiingilio kwenye mechi zote za ligi kuu ambazo zitachezwa kwenye uwanja wetu, hiyo inaanza kwenye mchezo wetu dhidi ya Dodoma Jiji FC ambapo tutakuwa tunachukua pointi zetu tatu muhimu.

“Mashabiki wanatakiwa kuja na jezi za Azam FC, waje waiyone timu yao na kusapoti kila mara. Hakuna tena kisingizio waje waone timu yao ikicheza kikubwa na kusaka alama zao tatu.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa