Baada ya Kufungiwa mechi tatu za Ligi Kuu , Mshambuliaji wa Yanga ambaye ni Raia wa Ghana Bernard Morrison hatimaye amemaliza kutumikia kifungo chake alichohukumiwa na bodi ya ligi baada ya mchezo wa Yanga dhidi ya AZAM FC.

Mechi ambazo amezikosa Morrison ni mechi kati ya Mtibwa Sugar, Ruvu Shooting, Simba SC na mechi dhidi ya KMC hakuwa sehemu ya kikosi cha Yanga.

 

Morrison Atoka Jela, Atuma Salama Geita Gold

Wakiwafuata Geita Gold jijini Mwanza, kikosi hicho cha Yanga kimewasili mapema hii leo, ambapo inatazamiwa mshambuliaji huyo atakuwa sehemu ya kikosi cha yanga kitakachovaana na wachimba dhahabu kutoka Geita.

Bernard Morrison alisajili kutokea Simba SC baada ya kuitumikia kwa misimu miwili wakati ambapo kabla ya kujiunga na Msimbazi alikuwa anawatumikia Wananchi na alihudumu kwa nusu msimu kabla ya kuisimamisha nchi kutokana na sakata lake la usajili kuwa na sintofahamu.

 

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa