Ongala Amsifia Dube

Kaimu Kocha Mkuu wa Azam, Kali Ongala amemsifia mshambuliaji wa kikosi hicho, Prince Dube kutokana na kiwango anachoonyesha.

Dube ambaye tangu msimu uliopita hakuwa kwenye kiwango bora kutokana na majeraha lakini jana katika mechi dhidi ya Simba alifunga bao pekee la ushindi.

Akizungumza baada ya kumalizika kwa mchezo huo, Ongala alisema: “Hatukuizingatia sana Simba bali sisi tulizingatia ni jinsi gani ambavyo tunaweza kupata ushindi.

“Dube ni mchezaji mzuri sana ambaye anaweza kukufungia magoli na sio hilo tu ni mtu ambaye anaweza kuipambania timu.

“Tunataka tuijenge timu kila mtu akipata nafasi aweze kuitumia vizuri kwa kutumia zaidi uwezo wake hivyo mchezo kama wa leo (jana) ni kwa ajili ya kujitangaza nje na ndani ya nchi.”

Acha ujumbe