Kocha Mkuu wa kikosi cha Simba, Juma Mgunda amepeleka lawama zake kwa mastraika wa timu hiyo kutokana na kushindwa kuzitumia nafasi walizopata.

Simba walipoteza mchezo wa ligi dhidi ya Azam jana alhamis kwenye Uwanja wa Mkapa, kwa bao 1-0 likifungwa na Prince Dube.

Mgunda, Mgunda Awashushia Lawama Washambuliaji Wake, Meridianbet

Akizungumzia matokeo hayo Mgunda alisema: “Kwanza namshukuru Mungu mchezo umemalizika salama, tumejitahidi kwa ajili ya kuhakikisha tunashinda mchezo lakini imeshindikana.

“Mchezo ulikuwa mzuri tumetengeneza nafasi nyingi za wazi lakini tumeshindwa kuzitumia, wenzetu wametengeneza nafasi na wameitumia hivyo ndivyo mpira wa miguu ulivyo.

“Tunarejea mazoezini kwa ajili ya kurekebisha hayo makosa yaliyojitokeza kwenye mchezo wa leo ili yasijirudie tena.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa