Yanga wanatarajia kuivaa Geita Gold kesho, wachezaji watatu wamejereshwa kwenye kikosi cha Yanga ambao ni Djuma Shaban, Fiston Mayele na Joyce Lomalisa.

Nyota hao hawakuonekana kwenye mchezo uliopita wa ligi dhidi ya KMC uliomalizika kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 lililofungwa na Feisal Salum.

yanga, Yanga Yawarejesha Kikosini Wachezaji Wake Watatu, Meridianbet

 

Sababu ya kukosekana kwa wachezaji hao ni kutokana na kusumbuliwa na majeraha hivyo tayari wameanza mazoezi.

Akizungumzia maandalizi yao, Kocha Msaidizi wa Yanga, Cedric Kaze alisema “Tunaingia kwenye mchezo wa kesho kwa tahadhari kubwa kutokana na ubora wa timu ambayo tunacheza nao.

“Geita Gold ni timu nzuri, tunajua mchezo utakuwa mgumu wa kushindana, Djuma Shaban, Fiston Mayele na Joyce Lomalisa wamerejea kwenye kikosi baada ya kupona.

“Tutawaangalia kama wapo fiti ili tuweze kuwatumia katika mchezo huo lakini hata wakikosekana tuna kikosi kipana na wachezaji waliopo wanaweza kucheza.”

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa