Vijana wa Mikel Arteta – Arsenal watakutana na kikosi cha Chelsea kinachonolewa na Frank Lampard katika fainali ya Kombe la FA Agosti 1, 2020.
Mchezo huo utawakutanisha makocha wawili wadogo kwenye Ligi Kuu Uingereza – Arteta (38) na Lampard (42). Mchezo huu utakuwa wa aina yake kutokana na uzoefu wa makocha hawa ambao kila mmoja ameshawahi kubeba Kombe la FA wakati walipokuwa wachezaji.

Lampard amebeba Kombe la FA mara 4 alipokuwa mchezaji wa Chelsea, wakati Arteta akilibeba kombe hilo mara 2 alipokuwa anaitumikia klabu ya Arsenal.
Arteta na Lampard wamekuwa na msimu mzuri kwenye Ligi Kuu – EPL wakijitahidi kuvinoa vikosi vyao. Uwezo wao wakuongoza vijana na kuwasimamia mchezaji mmoja mmoja lakini pia mbinu za matumaini na morali, zimewasaidia kwa kiasi kikubwa katika kazi zao kwa msimu huu.

Frank Lampard ambaye amekuwa akitumia mfumo wa 3-4-3 kwa kiasi kikubwa, ameweza kuingoza Chelsea mpaka kumaliza katika nafasi ya nne kwenye msimamo wa Ligi Kuu Uingereza- EPL na kufuzu hatua ya fainali ya Kombe la FA.
Japokuwa anaonekana ni kocha mtaratibu, Lampard amefanikiwa kutumia uwezo wake wa kuongoza wachezaji mmojammoja ndani na nje ya uwanja. Jambo hili limemsaidia katika kufanya maamuzi ambayo kwa namna moja ama nyingine yalimpatia matokeo katika michezo mbalimbali.

Mchezaji kama Olivier Giroud alionekana kama hana nafasi tena katika kikosi cha Chelsea na wengi kutazamia kuondoka kwa mshambuliaji huyo. Lampard amefanikiwa kwa kiasi kikubwa kurudisha morali na ari ya uchezaji wa Giroud na sasa tunamuona Giroud ambaye amekuwa akiongoza mashambulizi ya Chelsea na kuisaidia timu kupata matokeo.
Arteta nae amejitahidi kwa upande wake hasa tukiangazia suala zima la mchezaji Mesut Ozil ambaye amekuwa na wakati mgumu kwenye kikosi cha Arsenal kwa muda sasa. Arteta aliamua kumuacha Ozil katika mechi kadhaa, lengo likiwa ni kumpatia changamoto zaidi mchezaji huyo ambaye ni dhahiri ameshuka kiwango.

David Luiz ambaye ameonekana kushuka kiwango na kusababisha timu kukosa matokeo katika mechi muhimu kama ya Manchester City (3-0). Arteta amekuwa akimkingia kifua mchezaji huyo na kumuamini, Luiz alionesha uwezowake na kuisaidia timu yake kufuzu fainali ya Kombe la FA alipokutana na Manchester City katika nusu fainali na kushinda kwa magoli 2-0.

Arsenal na Chelsea watakutana tena katika dimba la Wembley mapema Agosti 1, 2020 watakapokuwa wakiwania Kombe la FA ambalo ni kombe muhimu kwa makocha hawa na timu wanazoziongoza. Kwa Arsenal, kubeba kombe hili itakuwa ni tiketi ya kushiriki michuano ya Europa msimu ujao na hivyo kuufanya mchezo huu kuwa na umuhimu wa aina yake.
Nini kinachokupa raha kama michezo ya kasino ya mtandaoni? Hasa unapojua kuwa kuna ushindi, jackpot na mizunguko kibao ya bure. Ungana na bwana Meridian kupata ushindi na burudani.


Mwajumah
Asante kwa makala nzuri#Meridianbettz
Sadick
Utakuwa usiku muhimu sana kwa wote wawili kuimarisha imani ya bodi na mashabiki kwao. Ni vigumu kutabiri nani mshindi mpaka dakika 90 zitakapotamatika#meridianbettz
Antony Luseno
Arsenal wamekuwa na msimu mbaya lakini cha ajabu wanaweza wakaibuka bingwa katika FA
Dorophina
Hii mechi sio ya kutabili mchawi dakika 90 maana inaonekana ngumu sana kila mmoja analitaka kombe la FA
Mwanahamisi
Asante kwa makala nzuri
Magdalena
Mtanange ninao usubuiria kwa hamu zote
Lydia Emmanuel Magoti
Mtanange huu usinipite navyo usubilia kwahamu utanipa pesa huu
Khadija
Huo mtanang’e nausubili kwa hamu#meridianbettz
Zeiyana
Luiz amekua na makosa mengi kipingi hiki ila arsenal wangempa mda tu
Caroline
Tunasubiri Kwa hamu
Fatina mfingi
Tunasubir kwa hamu cku ifike
Sauda
Tunasubiri
Janeflora malisa
Makala ipo powa
Fatuma kasomo
Vigumu kutabiri mshibdi mpira dakika 90
David Pere
Arteta hii mechi atashinda sababu Arsenal Wana history nzuri Sana katika hiki kombe la FA ushindi kwake ni lazimaa
Shafii
Ni mechi ya kukatana shoka hatumwii mtoto dukani.
Tatu
Tunasubili kwa hamu hii sio ya kukosa
Samiah
Nimechi kabambe
Isaya massawe
Kazi kwao sisi macho uwanjani tukishuhudia mtanange huu mkali
Franky
Good newz
Samira
Hii kali sana
Rehema
Gud news 👍
Furahav
Hii mechi sio ya kukosa.
Issa
Tutashuhudia fainali ngum na ya kuvutia hapa
Devotha
Hii mechi naitakia ushindi timu ya lampard naamini itafanya vema
Hope mwaikuka
Imeeleweka hii
Gabriel
Hapa n pata shika nguo kuchanika atumw mtt dukan
Tahiya
Ni vigumu kutabir mechi iyo
lombo
asante meridianbet kwa habar moto moto
farida ahmadi
Mechi kalii Sana ngoja tujionee wenyewe
Sabrina
Arsenal wakaze watufurahishe mashabiki
Salma ngende
Kazi ipo!
Genia Sikaluzwe
Hii mechi ni Kali Sana tunasubili kwa hamu
Latifa juma mohamed
Unasubirika kwa hamu japo mwamuz dkk 90
David Pere
Arteta hii mechi atashinda sababu Arsenal Wana history nzuri Sana katika hiki kombe la FA ushindi kwake ni lazimaa
Theckla
Chelsea anashinda hii mechi
Omary lukumbi
Hii itakua bonge la mecha sana kama wanakutana José morihno na asene wenger
tumaini
Maoni:Patachimbika
Povel
Gud news
felister
hapa leo nyasi lazima ziote moto
Amiri Kayera
Nyasi zitawaka
Asia Abdy
Wacha tuonee
Ester jackson
Utakuwa usiku muhimu sana kwa wote wawili kuimarisha imani ya bodi na mashabiki kwao
warda
Kweli kabisa hawa jamaa watangara sana badae