Azam Yataja Sababu ya Kuialika Zesco

UONGOZI wa Azam FC umefunguka sababu ya kuichagua timu ya Zesco katika tamasha lao la AZAMKA ni kutokana na hatua wanayoanzia kwenye michuano ya Shirikisho Afrika.

Tamasha la AZAMKA linatarajiwa kufanyika Agosti 14 mwaka huu kwenye Uwanja wa Azam Complex huku malengo yakiwa ni kuwatambulisha wachezaji wapya ndani ya kikosi hicho kwa mchezo wa kirafiki dhidi ya Zesco United kutoka Zambia.

Akizungumzia hilo, Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria ‘Zaka zakazi’ amesema kuwa sababu kubwa ya kuichagua Zesco ni kutokana na kuanzia raundi ya kwanza ya mashindano ya Shirikisho.

“Maandalizi yanaendelea vizuri na wapinzani wetu Zesco watakuja Dar Jumamosi, sababu ya kuichagua Zesco ni kutokana na wao wenyewe kuwa na sisi kwenye raundi ya kwanza ya mashindano ya kimataifa.

“Viingilio vya tamasha hilo vitakuwa kwa VIP A, 20,000 (ukitumia azampesa utanunua kwa 15,000), VIP B, 15,000 (kwa Azam pesa ni 10,000), VIP C 10,000 (kwa Azam pesa ni 7000) na Mzunguuko ni 5000 (kwa Azam pesa ni 3000).”

Acha ujumbe