EPL: Mambo Yananoga Kuelekea Katikati ya Msimu 2020/21.

Wiki hii tunaugawa msimu wa EPL. Kuelekea michezo ya wiki ya 19 kwa msimu wa 2020/21, mambo yanazidi kunoga.

Michezo iliyochezwa wikiendi iliyopita, imetoa picha nyingine kwenye msimamo na muenendo wa EPL msimu huu. Suluhu ya Liverpool vs Man United, ushindi wa Manchester City vs Crystal Palace, kipigo cha Sheffield United kutoka kwa Tottenham, Ushindi wa Leicester City vs Southampton na kipigo cha Fulham kutoka kwa Chelsea ni baadhi ya matokeo yaliyobadili muonekano wa msimamo wa ligi.

Nafasi 10 za juu kwenye msimamo wa Premier League kwa sasa.

United wanaendelea kuongoza ligi kwa tofauti ya pointi 2 dhidi ya Man City. Ikumbukwe, City wanamchezo mmoja pungufu ya United na matokeo ya ushindi kwenye mchezo walionao mkononi, yatawapandisha mpaka nafasi ya 1.

Liverpool anaporomoka mpaka nafasi ya 4 ikiwa ni matokeo ya kukosa ushindi kwenye michezo 4 mfululizo kwa mara ya kwanza kwenye EPL. Licha ya Leicester kushinda, bado anakibarua kizito cha kuendelea kukaa kwenye nafasi ya 3 kwani matokeo ya ushindi kwa Everton kwenye mchezo mmoja alionao mkononi, yatawaweka kwenye pointi sawa na kuendelea kumshusha zaidi Liverpool.

EPL
Nafasi za kati na mwisho kwenye msimamo wa EPL, 2020/21

Upande wa pili, kunatofauti ya pointi 2 tu kati ya Arsenal na Aston Villa katika nafasi ya 10 na 11. Villa anaakiba ya michezo 3 mkononi na hivyo endapo ataokota pointi zote 9 muhimu kwenye michezo hiyo, atapanda mpaka nafasi ya 2 au 3 (itategemea tofauti ya magoli).

Sheffield United bado jahazi linaendelea kuzama wakiwa wameshacheza michezo 19 na kushinda mchezo mmoja pekee. Ni tofauti ya pointi 4 tu kati ya Burnley na Fulham katika mstari wa nafasi za kushuka daraja. Timu zote (Burnley na Fulham) zinamichezo 2 pungufu ya Sheffield United.

Hali itakuaje kuelekea ungwe ya pili ya EPL msimu wa 2020/21. Unadhani timu zipi zitamaliza katika nafasi 4 za juu na kina nani watayaaga mashindano kwa msimu ujao??


USHINDI UPI NI MKUBWA KWAKO, £2,000,000? 🤑

Pokea mualiko wa Meridianbet na Pragmatic Play kutengeneza mkwanja kwenye kasino ya mtandaoni sasa. Jiunge sasa kupata ishindi huu.

INGIA MCHEZONI

15 Komentara

    Kweli EPL kumenoga

    Jibu

    Epl Mambo ni moto

    Jibu

    Mambo yote ni Epl

    Jibu

    Mambo ni 🔥🔥🔥

    Jibu

    Mambo yanazidi kutaradadi EPL

    Jibu

    EPL mambo yanazidi kusonga mbele

    Jibu

    Epl kumepamba moto

    Jibu

    EPL sio mchezo

    Jibu

    Burudan Kama zotee

    Jibu

    epl mambo ni moto

    Jibu

    EPL ngumu sana

    Jibu

    Epl ni moto sana

    Jibu

    Epl mambo ni motoo

    Jibu

    EPL kumenoga

    Jibu

    EPL kumekucha

    Jibu

Acha ujumbe