Shirika la utangazaji nchini Uingereza BBC limeiomba radhi klabu ya Manchester United baada  ya maneno ya kuikashifu klabu hiyo kuoneka kwenye matamgazo yao ambayo yalisomeka ‘Manchester United are rubbish’.

BBC wameeleza kuwa bahati mbaya hiyo imefanywa na mfanyakazi ambaye alikuwa anajifunza jinsi ya kurusha jumbe za maandishi za matangazo, halikuwa jambo walilodhamilia.

BBC
BBC NEWS

“Mapema leo, baadhi yenu mmeweza kuona kitu kidogo cha tofauti kwenye matangazo yetu ya maandishi chini ya screen ya matangazo ya habari, ambao uliandikwa kuhusu Manchester United, alisema mteangazi wa BBC.

“Natumai kwamba haikuwa kuwashutumu mashabiki wa Manchester United, Ngoja niwaelezee nini kilichotokea.

“Nyuma ya pazia, kuna mtu alikuwa anajifunza jinsi ya kuweka jumbe za matangazo ya maandishi, kwaiyo alikuwa anaandika tu pasipo mpangilio.

“Ndio jumbe hiyo ikaonekana kwaiyo tunaomba radhi kama umeona hilo na kuhisi umeonewa  na kwa mashabiki wa manchester United lakini hakika ilikuwa ni makosa na haikupaswa kuonekana kwenye screen.

“Hivyo ndivyo ilivyotokea, tunadhani ni bora tuelezee hilo kwenu.”


TENGENEZA FAIDA NA ZEUS ANCIENT FORTUNES

Una Kila sababu ya kufurahia wiki yako na kutengeneza mwaka huu uwe wa faida zaidi katika kasino zetu za mtandaoni za meridianbettz. Mchezo wa Zeus Ancient Fortunes unakuongoza kutekeleza hilo.

tetesi, Tetesi za Soka Barani Ulaya., Meridianbet

CHEZA HAPA

JIBU

Tafadhali andika maoni yako
Tafadhali andika jina lako hapa