Erasto Nyoni, Kinda Aliye Aminiwa na Maximo na Watanzania

Mwaka 2007 Tanzania iliishuhudia nafsi mpya inayokuja na dumu la petrol kwenye moto wa soka nchini. Alikuwa kijana mdogo tu wa miaka 19. Marcio Maximo alimuamini ugenini dhidi ya Burkina Faso. Na yeye hakumuangusha, aliifungia Tanzania bao la ushindi. Ni Erasto Edward Nyoni.

Erasto Nyoni

Ulikuwa mchezo wa kutafuta nafasi ya kufuzu michuano ya AFCON ya mwaka 2008 iliyokuwa ipigwe Ghana. Watanzania walikuwa hawamfahamu Nyoni ni nani. Nakumbuka hadi mtangazaji wa TVT siku ile Juma Nkamia alikosea, akasema mfungaji wa bao ni Haruna Moshi ‘Boban’ badala ya Erasto Nyoni. Kiukweli watanzania walikuwa hawamfahamu.

Kipindi hicho alikuwa anacheza Vitalo ya Burudani. Alikuwa ‘suprise package’ kwenye ukuta wa Nadir Haroub ‘Cannavaro’, Salum Swedi, Amir Maftah na Shadrack Nsajigwa ‘Fuso’ aliyekula umeme dakika ya 62. Ulikuwa mchezo wa kwanza wa timu ya taifa kwa Nyoni ila alicheza kama ana uzoefu wa mechi mia moja.

Erasto Nyoni


Alianza maisha yake ya soka katika academy ya Rolling Stone chini mzee Ally Mtumwa pale mjini Arusha. Baadae kocha wa AFC-ARUSHA, Madaraka Bendera akavutiwa na uwezo wake. Akamsajili ajiunge na timu ya watoto ya AFC. Baadae alijiunga na Vitalo baada ya AFC kushuka daraja. Azam walimrudisha nyumbani mwaka 2010. Miaka saba baadae akajiunga na pori lilipo makutano ya Uhuru na Msimbazi.

Nakumbuka free-kick yake ya kusawazisha pale Sudan kabla ya Ditram Nchimbi kutupa bao la ushindi la kutupeleka CHAN.

42 Komentara

    anakwenda na utamu wake nyoni mchezaji mwenye kipaji kikubwa kinachoisha ndani ya mipaka ya Tanzania

    Jibu

    Kiraka mwenye uwezo wake , nyoni nakubali Sana..mchezaji tegemeo timu ya simba sc & taifastars#meridianbettz

    Jibu

    Nakumbuka free-kick yake ya kusawazisha pale Sudan kabla ya Ditram Nchimbi kutupa bao la ushindi la kutupeleka chan #meridianbettz

    Jibu

    ana uwezo mzurii tu

    Jibu

    Nyoni yupo vizuri sana aisee ni vyema kuaminiwa

    Jibu

    Kijana yuko vizuri Sana

    Jibu

    Wa kawaida tu

    Jibu

    Hii ni mashine kwelikweli anapokiwa uwanai Basi nyavu zake haziguswi

    Jibu

    Iko poa sana

    Jibu

    Yuko vizuri sana nyoni.

    Jibu

    Nyoni aliwafanya watanzania wote kunyanyuka na kuweka bendeza juu ilikuwa furaha sana

    Jibu

    Yupo vizuri

    Jibu

    Kijana mahiriii sana anastahili pongezi kwakee

    Jibu

    Nyoni yuko poa

    Jibu

    Nakumbuka free-kick yake ya kusawazisha pale Sudan kabla ya Ditram Nchimbi kutupa bao la ushindi

    Jibu

    Erasto Yuko vizuri Sana

    Jibu

    Erasto nyoni mshamburiaji mzuri anajua mpambanaji apingwi

    Jibu

    Nyoni mchezaji hanayejua majukumu yake hanatisha sana

    Jibu

    Yuko poa tu mshikaj

    Jibu

    Erasto nyoni ni wakawaida sana

    Jibu

    Nyoni yuko vizuri

    Jibu

    Erasto nyoni##@%Erasto mashine

    Jibu

    Nyoni yuko vizuri sana

    Jibu

    Erasto namkubali sana

    Jibu

    Aliaminika ni kweli akaonesha uwezo

    Jibu

    nikikumbuka ile mechi ilikua ni ngumu sana, lakini kutokana na umakini wa erasto nyoni alibadilisha upepo baada ya kutupia goli ambalo lilimshangaza kila mmoja. #meridianbet

    Jibu

    Duuh!Erasto Nyoni yuko vizuri kwakweli ukilinganisha na umri wake bado unamruhusu kuendelea na makubwa kwenye soka ,akaze buti atafika mbali kama Samatta.

    Jibu

    Nyoni fundi sana

    Jibu

    Nyoni namkubali sana

    Jibu

    Erasto uyoooo

    Jibu

    Yuko vzr Sana hyu jamaa anajituma sana

    Jibu

    Sifa zote nampa erasto nyoni..ni mchezaji mzur sana kwangu

    Jibu

    Nyoni mnyama #Meridianbettz

    Jibu

    Erasto anauwezo mkubwa sana

    Jibu

    Nyoni mtu hatari

    Jibu

    Asanteni kwa habari meridian

    Jibu

    Ni namba 6 Mzuri sana hapa tanzania na anaitendea haki jezi ya timu yake

    Jibu

    Story ya kuvutia. Kwa sasa umri umemutupa mkono anakaribia kustaafu#meridianbettz

    Jibu

    Nyoni ni mtu hatari

    Jibu

    Kiraka anayejuah majukum yake uwanjan

    Jibu

    Ahsante kwa habari

    Jibu

Acha ujumbe

Meridianbet
Privacy Overview

This website uses cookies so that we can provide you with the best user experience possible. Cookie information is stored in your browser and performs functions such as recognising you when you return to our website and helping our team to understand which sections of the website you find most interesting and useful.